Meneja wa matawi ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi (kushoto) akimkabidhi hotuba yake Waziri wa Fedha Zanzibar- Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa aliyekua mgeni rasmi katika kongamano la Wadau wa Utalii Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa NMB – Philbert Casmir.
Meneja wa matawi ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi akizungumza kwenye kongamano la wadau wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATO) lililowaleta pamoja zaidi ya wadau 250 katika Hoteli ya Verde.
Benki
ya NMB imesema kuwa inathamini sana sekta ya utalii nchini na imeweka
mikakati endelevu zaidi katika kuhakikisha shughuli za utalii zinakuwa zaidi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa matawi ya Benki ya NMB Zanzibar
- Abdalla Duchi, wakati wa mkutano wa wadau wa utalii Zanzibar(ZATO)
uliofanyika visiwani humo kwa udhamini mkuu wa Benki ya NMB.
Alisema Benki hiyo imejipanga vyema kutoa suluhisho la
huduma za kifedha, kwa kuwa na mifumo bora zaidi ikiwemo ya ubadilishaji fedha
na Biashara ya kadi ambayo imewezesha wataliii kutohangaika
wanapofanya manunuzi na malipo mbali mbali kwa kushirikiana na mahoteli na
baadhi ya makampuni ya utalii, walihakikisha wana mashine za malipo (POS) na pia kuimarisha
mfumo wa malipo ya mitandano (E-Commerce).
Naye Mkuu wa Idara ya Biashara za kadi wa Benki
ya NMB - Philbert Casmir alisema wanaimarisha huduma hizo ili kuhakikisha
watalii wanapata huduma kupitia matawi ya Benki hio hasa pale yanapotokezea
majanga ikiwemo Covid - 19 ambayo ilisitisha huduma nyingi.
Philbert Alifafanua kuwa Benki hiyo inaelewa katika kipindi
cha Covid -19 biashara ikiwemo ya utalii na sekta ya hoteli zilipata
changamoto. Hivyo, NMB ipo karibu zaidi na wateja wao ili kuhimili changamoto
hizo zilizojitokeza.
Ametoa rai kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wajumbe wa
ZATO, na Wananchi wa Zanzibar kwa ujumla, kutumia Benki ya NMB kwani ipo kwa
ajili yao, na ina mifumo thabiti ya kutoa suluhisho la huduma za kibenki, na
ndiyo maana imetambuliwa na taasisi za kimatafa kama EURO Money kuwa ndio
benki bora zaidi hapa nchini kwa miaka minane mfulululizo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇