Mkuu wa Wilaya ya Kilombero – Ismail Mlawa (wa tatu kutoka kulia ) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mlimba Wilayani Kilombelo Mkoani Morogoro wakati wa hafla ya ufunguzi iliyofanyika jana. Kutoka kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Baraka, Ladislaus , Meneja wa tawi la NMB Mlimba – Omary Mtibiro, Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara – Salie Mlay , Meneja wa Kanda ya Mashariki – Dismas Prosper na Afisa Tarafa ya Mlimba – Emiliana Simanga.
Meneja wa tawi la NMB Mlimba – Omary Mtibiro (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero – Ismail Mlawa baada ya kuzindua rasmi tawi hilo jana.
………………………………………………………..
Benki ya NMB imefungua tawi jipya la Mlimba katika Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro. Tawil hili ni neema kwa wakazi wa eneo hili kwani walikuwa wakisafiri umbali wa kilomita 150 ili kuzifikia huduma za kibenki.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, kwa niaba ya Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Salie Mlay alisema ujenzi wa tawi hilo Mlimba ni utekelezaji wa sera ya Benki hiyo ya kuwasogezea wanachi huduma za kibenki.
Mlay alisema kuwa, NMB imeendelea kuimarisha huduma mbalimbali na mpaka sasa wameshafungua jumla ya matawi 12 Mkoani Morogoro – lengo likiwa kuhakikisha jamii inapata huduma za kibenki zilizo bora na kwa ukaribu zaidi.
Akizindua tawi hilo la NMB Mlimba, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero- Ismail Mlawa alisema, ujenzi huo ni sehemu ya ushahidi wa Serikali kumletea mwanachi maendeleo ili aweze kuondokana na changamoto zinazomzunguka na kuwataka wafanyabiashara kuitumia Benki hiyo kwaajili ya kufanya maendeleo.
Kwa niaba ya wafanyabiashara – Joyce Chaula ameishukuru Benki ya NMB kwa kuwasogezea huduma, kwani wanaamini watanufaika ikiwemo fedha zao kuwa salama na hata wao wenyewe kuweza kupata mikopo ili kukuza biashara.
Katika uzinduzi huo NMB imetoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni tano ikiwa ni mabati kwaajili ya uwezekaji wa shule ya Sekondari ya Kalengakelu iliyopo Tarafa ya Mlimba hii ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇