Waziri wa Fedha na Mipango- Dk Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 15.2 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB – Dk. Edwin Mhede (wa pili kutoka kushoto) ikiwa ni gawio kwa Serikali wakati wa hafla iliyofanyika jana Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB - Ruth Zaipuna na wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango - Mary Maganga na wa kwanza kutoka kulia ni Msajili wa Hazina - Athumani Mbuttuka.
Waziri wa Fedha na Mipango - Dk. Philip Mpango akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 16 Afisa wa Ubalozi wa Uholanzi nchini - Mathis van Eeuwen (kushoto) iliyotolewa na Benki ya NMB kwa Rabo Bank Group. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Msajili wa Hazina - Athumani Mbuttuka, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB – Dk. Edwin Mhede na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo - Ruth Zaipuna.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB - Ruth Zaipuna alisema kuwa,
fedha zilizokabidhiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana katika mwaka wa fedha
2019 baada ya kuondoa gharama na kodi ambayo ilikiwa shilingi 45 bilioni.
Zaipuna amesema mbia mwingine ni Benki ya Rabo ya nchini
Uholanzi ambayo imepata gawio la shilingi 16. 8 bilioni huku shilingi 16 bilioni zikienda kwa wawekezaji wengine ikiwemo taasisi za serikali. Alisema
kwa mwaka 2019 licha ya benki kuwa chini ya uongozi wa mpito, lakini iliendelea
kufanya vizuri na hata kipindi cha corona bado waliendelea kufanya vizuri kwani
katika nusu ya mwaka wa fedha 2020 NMB wameshasajili faida ya shilingi 93
bilioni.
Kwa mujibu wa mtendaji huyo, wameshaanza mkakati wa kuinua
kilimo nchini na tayari wamekopesha wakulima shilingi 800 bilioni huku
wafanyabiashara wakikopa shilingi 2.2 trilioni. Nyingine ni ununuzi wa madawati
40,000 na kompyuta 1000 zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia shule mbalimbali na
kuwa wameendelea kuwa benki bora kwenye tuzo za jarida la kimataifa la Euro
Money kwa miaka 8 mfululizo.
Akipokea mfano wa hundi hiyo, Waziri wa Fedha - Dk. Philip
Mpango alisema kiwango kilichotolewa ni kizuri na kuna matumaini makubwa ya
gawio kupanda kwa mwaka huu. Dk. Mpango aliitaja Benki ya NMB kuwa miongoni mwa
taasisi zinazofanya vizuri zaidi.
Awali Mwenyekiti wa bodi ya NMB Dk Edwin Mhede aliahidi Benki
hiyo itafanya vizuri zaidi mwaka ujao baada ya kupata Afisa Mtendaji Mkuu kwani
alipokuwa akikaimu hakuwa na nguvu zaidi katika maamuzi, Hivyo, wanaamini benki
hiyo itaendelea kuwa imara zaidi na kuwa mfano kwa mabenki mengine nchini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇