Mamlaka ya Usalama wa Anga (TCAA) imezuia ndege za AirKenya Express, Fly540 na Safarilink Aviation kutua nchini, Agosti 01, ndege za Kenya Airways zilipigwa marufuku kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amethibitisha hilo akisema ndege hizo 3 zimezuiwa kufuatia mgogoro unaoendelea baina ya mataifa hayo.
Wiki iliyopita, Kenya ilitangaza nchi 130 ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia bila masharti ya kukaa karantini na Tanzania haikuwepo katika orodha.
Johari amesema zuio la ndege hizo nne halitaondolewa mpaka wasafiri kutoka Tanzania wakijumuishwa kwenye orodha ya raia ambao hawatolazimika kukaa karantini.
Ameongeza kuwa inashangaza Tanzania ambayo ni salama dhidi ya mlipuko wa Corona Virus haipo kwenye orodha ya Kenya
.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇