Mgombea ubunge wa Jimbo la Kasulu Mjini kupitia CCM, Profesa Joyce Ndalichako anawaalika wananchi kuhudhuria kwa wingi katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zitakazofanyika kuanzia saa 4 asubuhi Jumamosi Septemba 5, mwaka huu, kwenye Uwanja wa CCM Umoja Kasulu Mjini.
Prof. Ndalichako ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,anawaomba wananchi wasikose kwenye mkutano huo muhimu, kwani kuna mambo mengi atakayowaeleza ikiwemo mikakakati mbalimbali atakayoifanya yeye na Serikali ya CCM kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo endapo watamchagua yeye, madiwani wa CCM na mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli. Kauli mbiu yake ya; UWAJIBIKAJI KWA MAENDELEO KASULU MJINI inaakisi mikakati hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇