Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akiongoza kikao cha kujadili na kupitia Miundo ya Taasisi ( organization structures ) ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya wizara hiyo, Dk. Maurus Msuha.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi za Uhifadhi za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Kikao hicho kimefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi- Rasilimaliwatu Witness Shoo ( aliyesimama ) akijibu swali lililohitaji ufafanuzi kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha ( aliyevaa uniform za JWTZ wa tatu kutoka kushoto kwa Witness Shoo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akifurahia jambo kufuatia michango ya wajumbe iliyokuwa ikitolewa wakati wa kikao chake na Makamishna wa Uhifadhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini, wakimsikiliza kwa umakini Naibu Katibu Mkuu Dkt. Allan Kijazi wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Fredy Manongi, akisisitiza kuhusu utekelezaji wa sheria kwa watumishi wa Jeshi la Uhifadhi ili kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya katika nyanja zote.
Baadhi ya wakuu wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, wakifuatilia kwa ukaribu kikao cha kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi- Rasilimaliwatu Witness Shoo ( aliyesimama ) akijibu swali lililohitaji ufafanuzi kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha ..
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇