LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 8, 2020

'KAWE DAY' YA SHULE YA SEKONDARI KAWE UKWAMANI JIJINI DAR ES SALAAM, YATIA FORA

 
Na Bashir Nkoromo, Kawe

Maadhimisho ya siku ya kuanzishwa rasmi Shule ya Sekondari ya Kawe Ukwamani iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, 'Kawe Day' yaliyofanyika leo, Ijumaa, Agosti 7, 2020, katika shule hiyo yametia fora baada ya kufanyika kwa ufanisi mkubwa.


Maadhimisho hayo yaliyoanza saa 2 asubuhi  yalionyesha kufana kutokana na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo wazazi, wakuu wa shule jirani, viongozi wa ngazi mbalimbali katika Kata ya Kawe na Wadau wa maendeleo ya shule hiyo.


Sanjari na mahudhurio, Maadhimisho hayo yalinoga kutokana na Maonesho ya kitaaluma yaliyoanaliwa na walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa umahiri mkubwa na hasa jinsi wanafunzi katika Idara mbalimbali za masomo walivyokuwa wakieleza mambo kadhaa kwa umahiri mkubwa kila mmoja katika eneo la fani ya somo alikopangiwa.


Licha ya fani zote kuwa kivutio, lakini maonyesho kuhusu ujasiriamali na ya Sayansi yalionyesha kuvutia wengi kiasi cha kuwashangaza baadhi ya wageni baada ya kushuhudia umahiri walioonyesha wanafunzi katika kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo za batiki, vinywaji baridi, sabuni za kufulia na za kutakasa mikono kwa kutumia tekonolojia rahisi lakini ya kisasa.


Kuvutia kwa Maadhimisho hayo kulisababisha baadhi ya wazazi hasa wadau wa maendeleo kuamua kuisaidia shule kutatua baadhi ya changamoto huku zingine wakiahidi kuzifanyika kazi kwa kutafuta marafiki watakaokuwa tayari kuzitatua.


Mmoja wa Wadau aliyeonyesha kuguswa ni Davidi Kayuni ambaye aliahidi kuipatia shule kompyuta tano ili kupunguza au kutatua changamoto ya shule hiyo ya kuwa na kompyuta moja tu na hivyo kukwama katika uchapaji wa kazi mbalimbali.


"Baada ya kuona maonyesho yenu, kwa kweli nimeiona kesho yenu ya kuwa wahandisi na wajasiriamali watakaotufikisha kwenye kuunga mkono mwito wa Rais wetu Dk. Magufuli wa kuhakikisha  Tanzania inakuwa ya uchumi wa viwanda. Kwa sababu hiyo mimi kama mdau wa maendeleo, nitaipatia shule hii kompyuta tano  ili mzitumie kutafuta kwa njia ya mtandao mambo hahusuyo masomo kwa njia za kisasa", alisema Kayuni.


Mapema,  akizungumza  shuleni hapo, Mkuu wa shule hiyo Safina Egha, amesema, shule hiyo iliyoanzishwa  Aprili 16, 2006 ikiwa na wananfunzi 320 na walimu sita ikiwa na majengo mawili yenye vyumba sita, kimoja kikitumika kama ofisi na vitano madarasa ya kufundishia, ina majengo tisa, ikiwemo la maabara, la Maktaba na chumba cha huduma ya kwanza  na faragha kwa wasichana.


Alisema, shule sasa ina walimu  42, walimu 15 wanaojitolea na walimu 26 wa mazoezi, mtaalamu mmoja wa maabara, walinzi watatu,  huku shule ikiwa na jumla ya wananfunzi 1280 ambao kati yao wasichana ni 617.


Mkuu wa shule hiyo alizitaja changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni  pamoja na ukosefu wa kompyuta, akisema iliyopo ni moja ambayo inatumiwa na Utawala na  na Taaluma na hivyo kusababisha ucheleweshaji wa kazi za kila siku na kwamba shule inayo mashine ya kurudufia ambayo bado inadaiwa malipo yake.


Alisema changamoto nyingine ni shule kuwa na matundu machache ya vyoo kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo na pia baadhi ya sehemu za shule hazina uzio hivyo walimu kulazimika kutumia muda mwingi kuwachunga watoto.


Mkuu huyo wa shule alisema, kwa kuwa shule hiyo imeweka lengo la kupandisha ufaulu kwa asilimia 95 na kupunguza alama 0 kutoka digiti 2 hadi digiti moja na kufuta daraja sifuri kabisa,  hivyo ni muhimu sana  wadau wa elimu na Mamlaka husika kutoka kipaumbele katika kusaidia kuondoa changamoto zote ambazo ni tishio katika  utoaji wa elimu na makuzi  ya wanafunzi.


Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa Katibu wa CCM Kata ya Kawe, Fatma Awadhi ambaye katika hotuba yake alitoa mwito kwa wadau kuendelea kusaidia shule mbalimbali zilizomo katika Kata hiyo hasa zile zinazoonyesha uhitaji mkubwa kama Kawe Ukwamani.


Fatma ambaye alifuatana na viongozi kadhaa wa CCm katika Kata hiyo aliahidi kuwa karibu na uongozi wa Kawe Ukwamani kwa kuzichukua changamoto na kuzipeleka ngazi za juu ili kupatiwa majibu.


Mwishoni, Mkuu wa taaluma wa shule hiyo Mwalimu Chacha alitangaza wanafunzi na walimu bora na kupatiwa zawadi mbalimbali kufanya vizuri zaidi katika matokeo ya mitihani mitihani mbalimbali, ambapo kwa kitacho cha chanza walipatiwa zawadi kutokana na kuwa katika tatu bora kuwa ni 1. Josephati Peter  2. Baraka Makali 3. Christian Mwaisapula.

Kwa kidato cha Pili ni 1. Vitalisi Kimario, 2. Abubakari Mkamba, 3. Michael Marashi na Kidaco cha Tatu kuwataja kuwa ni 1Elvin Valentino, 2. Baraka Kulembelwa, 3.Rebecca Martin, huku Kidato cha Nne wakiwa ni 1.Bushir Mataja, 2. Tamia Msonda na 3.Irene Nyamhanga. Kwa picha motomoto za Maadhimisho hayo, tafadhali >>BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages