Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodom,
Mustapher Shaaban akitoa hotuba ya Swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi
Jijini Dodoma baada ya swala ya Eid.
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakiongoza takibira kabla ya Swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma .
Mwandishi wa Habari wa Shirika la
Utangazaji la BBC,Aboubakari Famau (kwanza Kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na Mhariri wa Fullshangwe blog, Majid Abdulkarim na mbele ni
Mtoto wake Famau baada ya Swala ya Eid iliyofanyika katika Msikiti wa
Gadafi Jijini Dodoma.
Baadhi ya waumini wakifatilia kwa umakini hotuba ya swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi leo Jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari wa Shirika la
Utangazaji la BBC, Aboubakari Famau Kushoto) akisalimiana na
Mhariri wa Fullshangwe blog, Majid Abdulkarim leo baada ya swala ya Eid
katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma.
……………………………………………………..
Na Majid Abdulkarim, Dodoma
Waumini wa Dini ya Kislamu nchini
wametakiwa kuliombea taifa kudumisha amani na utulivu uliyopo hasa
katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika 28 Oktoba
2020 ili kuweza kupata viongozi bora , waadilifu na wazalendo katika
kuwatumikia watanzania kwa kuleta maendeleo.
Wito huo umetolewa na Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Dodom, Mustapher Shaaban katika Msikiti wa Gadafi Jijini
Dodoma wakati wa swala ya Eid.
“Hivyo maombi hayo yatasaidia
kupata viongoz waadilifu, wema , wanyenyekevu ,wanao sikiliza wananchi
wao, wenye uzalendo na kutatua kero za watanzania kwa wakati bila
kuleta uvunjifu wa amani na mshikamano uliopo katika nchi yetu”,
ameeleza Sheikh Shaaban.
Mbali na hilo Sheikh Shaaban
amesema dini ya uislam inafundisha amani na mshikamano hivyo ni vema
kupeana ushirikiano kwa ustawi wa amani na maendeleo nchini ili kujenga
taifa bora.
Aidha Sheikh Shaabani amewataka
wamini hao kutumia siku ya Eid kuwaombea ndugu na marafiki wote
waliyotangulia mbele za haki kusamehewa makosa yao yote kwa Mwenyezi
Mungu na kusema mambo mazuri juu yao ili kupata kauli thabit kwa Allah.
Pia Sheikh Shaabani amekumbushia
kuwa leo ndo siku muhimu watu wanatakiwa kukaa na familia zao kwa
kujumuika na kufanya ibada, ya kuchinja kwa wale wenye uwezo wa kuchinja
na kutoa sadaka kwa watu wasio kuwa nauwezo ili kutimiza adhima ya siku
kuu ya Eid.
Sheikh Shaabani amemaliza kwa
kutoa pole kwa Taifa kwa kumpoteza Hayati Benjamini Mkapa aliyekuwa Rais
wa Awamu ya Tatu na kusema kuwa waumini wa Dini ya Kislamu watamuenzi
kwa mambo mengi ikiwemo Ujenzi wa Msikiti wa Gadafi ulijengwa kipindi
cha Utawala wake na kipindi hicho aliyatoa majengo ya kilichokuwa Chuo
cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha
Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
“Hivyo waumini tunamuenzi Hayati
Mkapa kwa hayo mambo mawili makubwa kwani leo tumepata ibada yetu ya
swala ya Eid hapa na watoto wetu wanaendelea kupata elimu Chuoni hapo na
wanapomaliza masomo yao wanapata ajira na kulitumikia taifa”, ameweka
wazi Sheikh Shaaban.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇