*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wananchi wameungana na viongozi
mbalimbali wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika misa ya kumuaga Rais Mstaafu
wa awamu ya Tatu Hayati Benjamin Wiliam Mkapa katika uwaja wa Uhuru
JIjini Dar es Salaam.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa na
Mwanafamilia wakati wa Misa ya kumuaga Rais Mstaafu Hayati Benjamin
William Mkapa imesema Sababu ya kifo chake ni Mshituko wa Moyo.
Akizungumza katika misa hiyo
Msemaji wa Familia Bw.William Erio amesema kuwa mzee wetu alikuwa
hajisikii vizuri akaamua kwenda hospitali na baada ya vipimo alionekana
kuwa ana ugonjwa wa Maralia hivyo akalazwa kwa siku hiyo na Alhamisi
mchana aliendelea vizuri na baadae usiku alipatwa na mshtuko akafariki
dunia ikisemekana chanzo cha kifo chake ni Ugonjwa wa Moyo.
“Alikuwa anasikiliza taarifa ya
habari na baadae alitaka kuinuka kukaa akainamisha kichwa na hiyo mpaka
walipokuja kumpima akawa amethibitika kwamba amefariki, sababu yake ya
kifo alipata mshituko wa moyo”. Amesema Bw.Erio.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇