LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 9, 2020

WANAHABARI WAFURAHISHWA NA MAFUNZO YA JINSI YA KURIPOTI HABARI ZA MKUTANO MKUU WA CCM

 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG), Ernest Sungura akifafanua jambo jinsi ya kuandika habari kwa ufasaha kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Taratibu  pamoja na Destuli na Utamaduni wa  Chama Cha Mapinduzi  (CCM), wakati  wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho unaofanyika kwa siku mbili  Julai 11 -12, 2020 jijini Dodoma. 

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waripoti kwa usahihi matukio muhimu ya mkutano huo. Wakufunzi wengine waliotoa maada ni; Mwanzo Millinga Mhariri wa Mitandao ya Kijamii (UMG), Josephat Mwanzi, Msaidizi wa CEO Kimkakati (UMG). PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-CCM BLOG



 Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mafunzo hayo
 Jasmane Shamwepo Mtangazaji wa Kituo cha Radio cha Mwangaza FM, akieleza jinsi alivyofurahishwa na mafunzo hayo yaliyomwezesha kupata uelewa kuhusu Katiba ya CCM  na utaratibu  wa mkutano mkuu.
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira, akielezea jinsi mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza kwa wanahabari, jinsi yalivyomfumbua kwa kujua mambo mengi kuhusu Katiba ya chama hicho, hivyo kumsaidia kuandika kwa ufasaha habari za mkutano huo.
 Anastazia Anyimike wa Habari Leo
 Sakina Masoud wa Uhuru FM, Inayomilikiwa na CCM
 Agusta Njoji wa Nipashe
 Mwanahabari Saida Issa wa Gazeti la Zanzibar Leo
 Oliver Nyeriga EATV na EARADIO
 Joyce Mwakalinga wa Azam TV
 Happy Mtweve wa Gazeti la Uhuru
 Mpiga Picha wa Gazeti la Daily News, Iddy Mwema
 Fred Alfred wa Gazeti la Uhuru
 Josephine Kaponya wa EFM na TVE
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa UMG, Ernest Sungura, akihitimisha mafunzo hayo na kuahidi maoni mbalimbali yaliyotolewa na wanahabari katika mafunzo hayo, kuyawasilisha kwa uongozi wa CCM ili yafanyiwe kazi kwa lengo kwamba siku za usoni kuwepo na utaratibu mzuri wa kuendesha mafunzo ya namna hiyo.
 Aboubakar Famau wa BBC
 Mwanahabari mkongwe wa Gazeti la Uhuru, Bakari Mkondo, aliwataka wanahabari kuacha tabia ya kuandika habari kwa chuki bali waandike kwa kufuata maadili ya uandishi bila upendeleo


NA MWANDISHI WETU
BAADHI ya waandishi wa habari watakaoripoti habari na matukio ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kufanyika kuanzia kesho hadi kesho kutwa, wamesema mafunzo ya namna ya kuripoti mkutano huo yamewajengea uelewa utakaowawezesha kuhabarisha umma kwa ufasaha na ueledi.

Wamesema mafunzo ya aina hiyo ni yakwanza kupewa, hivyo yamewajengea uwezo zaidi, kujiamini na kufahamu baadhi ya mambo ya msingi kuhusu mkutano huo wa ngazi ya juu wa CCM.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika jana jijini hapa katika Ofisi za Uhuru Media Group (UMG) zilizopo Area C, Richard Mwaikenda, mwandishi kutoka Blogu ya CCM, alisema licha ya ukongwe wake kwenye tasnia ya habari lakini ni mara ya kwanza kupatiwa mafunzo hayo.

“Wengi waandishi wa habari wanachojua ni kuandika habari, lakini kufahamu mambo ya msingi kuhusu CCM baadhi hawajua hata Ilani au Katiba ya CCM inasemaje. Kutofahamu mambo hayo kunajenga ukakasi kama mwandishi anauwezo wa kuandika habari kuhusu CCM,” alieleza.

Alisema waandishi wa habari wanapaswa kufahamu kusoma maandiko mbalimbali ya chama kutawajengea uwezo wa kuchambua na kuandika habari zinazohusu CCM.
Naye, mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Aboubakar Famau, alisema waandishi wa habari bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo za kiusalama.

Alisema mwandishi anapokwenda kuripoti habari kuhusu chama cha siasa lazima masuala ya usalama wake uzingatiwe ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha.

Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Nipashe, Agusta Njoji, alisema mafunzo hayo yamewaongezea maarifa yatakayowawezesha kuandika habari kutoka vyanzo sahihi.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari  Mkoa wa Dodoma (CPC) Mussa Yusuph, alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa mwandishi wa habari kwani kabla hajaripoti habari kuhusu tukio lolote la kisiasa, kuna mambo ya msingi anapaswa kuyazingatia.

Aliyataja mambo hayo kwanza ni lazima mwandishi afahamu kwa undani katiba, kanuni, sera na ilani ya chama husika  na mienendo na tabia za wanachama wake.

“Pia mwandishi wa habari anatakiwa kufahamu mazingira ya eneo ambalo anakwenda kuchukua habari hususani usalama wa eneo, aina gani ya nguo anazopaswa kuvaa na ajizuie kuegemea upande wowote bali aripoti kwa kuzingatia msingi ya taaluma inavyomtaka,” alibainisha.

Akitoa mada kwenye mafunzo hayo yalioandaliwa na Uhuru Media Group (UMG) ikishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC), Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa UMG, Ernest Sungura, alisema kuna baadhi ya mambo ambayo waandishi wengi wamekuwa wakiyaandika kuhusiana na Mkutano Mkuu wa CCM wakiwa hawana uelewa wa kutosha.

“Ni vyema tutakapoenda kuandika habari za mkutano mkuu, kuna mambo ambayo tuwe na uelewa nayo na kuwa na taarifa rasmi kutoka kwa wahusika,” alisema Sungura.
Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanandika habari za Mkutano Mkuu huo kwa usahihi na umakini.

Mtangazaji wa kituo cha luninga cha Azam, Joyce Mwakalinga, aliishukuru UMG na CPC, kuandaa mafunzo hayo kwani kuna mengi ameyafahamu ambayo awali hakuwa na uelewa nayo.

“Pia kuwafanya wajue katiba ya CCM waelewe nini maana ya Mkutano Mkuu na taratibu wake kwa uhakika na usahihi mzuri zaidi”

Mkuu wa Kanda zote kutoka UMG, Kiondo Mshana, alisema katika mkutano huo waandishi waweke uzalendo mbele.
“Tusiende kuandika mkutano huu tukiwa na agenda zetu binafsi mkononi au mtu fulani tufuate maadili ya kazi zetu,” alisema.


Kwa upande wake, Mhariri wa Mitandao ya Kijamii wa UMG, Mwanzo Millinga, alisema bado waandishi wa habari wana changamoto nyingi ikiwemo usalama wa waandishi wa habari wakati wakitekeleza majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages