Wakili
wa Kujitegemea James Marenga wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa
Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu
(DDA) unaotekelezwa na Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala
(Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini
kilichofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel jijini Dodoma.
Wakili wa Kujitegemea James
Marenga wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa
Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unaotekelezwa na Waandishi
wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online
TV) kilichofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel jijini Dodoma.
Wakili wa Kujitegemea James Marenga akiwasisitiza Waandishi wa Habari Mtandaoni kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (Arusha Press Club – APC) ambayo ni msimamizi wa mradi, Claud Gwandu akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) ambapo aliwataka
Waandishi wa Habari kufuata sheria zilizipo hata kama hawakubaliani
nazo wakati asasi zao zikiwasiliana na Serikali kuangalia namna bora ya
kurekebiha sheria hizo.
Mwenyekiti
wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (Arusha Press Club –
APC) ambayo ni msimamizi wa mradi, Claud Gwandu akizungumza wakati wa
Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu
kwa kutumia takwimu (DDA).
Mwenyekiti
wa Waandishi wa Habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media)
kupitia mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia
takwimu (DDA), Midraji Ibrahim akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).
Afisa Mipango wa Arusha Press Club, Seif Mangwangi akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).
Afisa Programu wa Mradi
wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA)
kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kutoka taasisi za
Freedom House, Lina Muro akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) wakiwa katika picha ya pamoja.

………………………………………………………………………………
Waandishi
wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/
Online TV) wametakiwa kuwa mstari wa mbele zaidi kuzingatia maadili ya
uandishi wa habari ikiwamo kuandika habari za ukweli na uhakika ili
kuepusha upotoshaji na kujiingiza katika migogoro.
Rai hiyo imetolewa leo Jumatatu
Julai 27,2020 na Wakili wa Kujitegemea James Marenga wakati wa Kikao cha
Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa
kutumia takwimu (DDA) unaotekelezwa na Waandishi wa habari wa vyombo vya
habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa
mbalimbali nchini kilichofanyika ukumbi wa Royal Village Hotel jijini
Dodoma.
Marenga alisema kati ya
waandishi wa habari wanaotakiwa kuandika habari kwa usawa na ukweli
zaidi ni waandishi wa habari wa mtandaoni kwa sababu wao wamekuwa
wakiripoti matukio papo hapo mara tu matukio yanapotokea.
“Kama unaandika habari
mtandaoni suala la maadili ya uandishi wa habari ni muhimu sana na
haliepukiki. Waandishi wa habari Mtandaoni ambao wanajulikana kama ni
Waandishi wa habari za Chap Chap mtandaoni wanatakiwa kuwa mstari wa
mbele kusimamia maadili ya uandishi wa habari ikiwemo kuandika habari za
ukweli na uhakika ili kuepuka kujiingiza katika matatizo”,alisema Marenga.
Pia, Marenga aliwataka waandishi
wa habari kutochanganya uandishi wa habari na siasa huku akisisitiza
kuwa endapo mwandishi wa habari anataka kujihusisha na masuala ya siasa
basi aachane na uandishi wa habari.
Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa
Arusha (Arusha Press Club – APC) ambayo ni msimamizi wa mradi, Claud
Gwandu aliwataka Waandishi wa Habari kufuata sheria zilizipo hata kama
hawakubaliani nazo wakati asasi zao zikiwasiliana na Serikali kuangalia
namna bora ya kurekebisha sheria hizo.
Awali, Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari wa vyombo vya
habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi
wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim
aliwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi wa
habari hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu nchini
Tanzania.
Afisa Mipango wa Arusha Press
Club, Seif Mangwangi alisema miongoni mwa malengo ya kikao hicho cha
Midterm Review ni kupitia mafanikio, changamoto na matarajio ya baadae
ya mradi tangu ulipoanza Machi 2019, wanakundi kutunga kanuni na
mwongozo zitakazosimamia kundi hilo la waandishi wa habari mtandaoni ili
kutoa matokeo yanayotarajiwa na kupitia mwongozo wa wanahabari
watakaokuwa wakiutumia kwenye shughuli zao za kila siku za kihabari
ambao umetengenezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.
Alisema kikao hicho ni sehemu ya
utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa
kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative
Media) unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia
taasisi za Freedom House pamoja na PACT na unasimamiwa na Klabu ya
Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (APC).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇