Na Mwandishi wetu, Bukoba.
Shirika la viwango Tanzania TBS limeendesha mafunzo
maalumu ya ujasiliamali na umuhimu wa ubora wa bidhaa
kwa wajasiliamali mkoani Kagera kwa lengo la kuboresha
bidhaa zao ili kuendana na ushindani wa soko la dunia.
Mafunzo hayo yamefanyika julai 27,mwaka huu katika
ukumbi wa Bukoba hotel ambayo yamewahusisha
wajasiliamali Zaidi ya 50 kutoka wilaya za mkoa huo
ambapo wajasiliamali hao wameelezwa umuhimu wa kuwa na
alama ya ubora(TBS) kwenye bidhaa zao.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amelishukuru shirika hilo kwa kuamua kuwafikia wajasiliamali kwenye maeneo yao na kuweza kuzijua changamoto zao katika usindikaji wa bidhaa zao.
Kinawiro amesema kuwa wajasiliamali ni watu muhimu katika
ukuaji wa uchumi wa taifa ambao wanatakiwa kusaidiwa kwa
kupewa elimu ya ujasiliamali pamoja na namna bora ya
utunzaji wa bidhaa tangu zikiwa malighafi hadi kufikia hatua ya
kwenda sokoni.
“Wajasiliamali ni watu muhimu kwa taifa letu, TBS mnalo
jukumu kubwa sana la kuhakikisha wadau hawa wanapata
elimu sahihi na bora yenye lengo la kuwainua katika shughuli
zao, tunaona sasa nchi yetu imefikia uchumi wa kati mchango wa watu hawa upo mkubwa.” Ameeleza Kinawiro.
Ameongeza kuwa mkoa wa Kagera unapakana na nchi
takribani nne ambazo zinaweza kuwa fursa kwa wajasiliamali
wa mkoa huo hivyo wajasiliamali wakikosa alama za ubora
kwenye bidhaa zao watakosa masoko kwenye nchi hizo
kwakuwa zitakuwa hata hazitambuliki hata kama ni nzuri.
Aidha Kinawiro amewataka SIDO na TBS kuwasaidia
wajasiliamali kupata vifungashio bora ili kuweza kuuza bidhaa
zao kwa usafi na ubora na pia waweze kupata faida ambapo
amesema kuwa changamoto hiyo imekuwa kero na kuwafanya wajasiliamali kutumia vifungashio vivyobora na kuwapelekea walaji kushindwa kununua bidhaa zao.
Hamisi Sudi ni meneja utafiti na mafunzo kutoka TBS akiongea
kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa shirika hilo amesema kuwa
wamekuwa wakitoa mafunzo hayo mara kawa mara kwa
wajasiliamali nchini lengo ni kuwawwezesha kuzalisha bidhaa
zenye ushindani kwenye soko la dunia.
Ameeleza kuwa shirika hilo linaendelea kupambana ili
kuhakikisha wajasiliamali wote nchini wanakuwa na alama za
ubora (TBS) kwenye bidhaa zao ili kumridhisha mlaji wa
mwisho kuiamini bidhaa hiyo kutokana na uwepo wa alama
hiyo.
Bw.Sudi ameongeza kuwa zipo changamoto kwa wajasiliamali
wanaoshindwa kukidhi vigezo vya kuweza kupewa alama na
badala yake wanapeleka bidhaa zao sokoni huku wakijua
hazina ubora uliothibitiwa na mamlaka husika ambalo suala
hilo huwapelekea kukosa masoko ya ndani nan je ya nchi kwa
ujumla.
Amewataka wajasiliamali kuwa na tabia ya kuhudhuria
mafunzo mbalimbali yanayotolewa na shirika hilo ili kuweza
kuwajengea uwezo binafsi wa kuzalisha bidhaa zilizo bora na
kuweza kupata masoko makubwa nay a kuaminika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wajasiliamali
waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo
waliyoyapata yatawasaidia kuanza kuzalisha bidhaa zenye
ubora Zaidi na kuweza kupata masoko makubwa.
Matungwa Daniel ni mkurugenzi wa kiwanda cha Nyaka
Food kilichopo Manispaa ya Bukoba ambaye amesema kuwa
amekuwa akipata changamoto ya kuuza bidhaa zake nje ya
nchi kutokana na bidhaa zake kutokuwa na alama ya ubora
(TBS) suala linalompelekea kukosa masoko licha ya kuwa
watu kutoka nchi za nje wanazipenda bidhaa zake.
Ameongeza kuwa serikali ikiwasaidia wajasiliamali hao kupata alama ya ubora kwa haraka itawasaidia kupata masoko na kupunguza usumbufu kwao pale wanapokwenda kuuza bidhaa hizo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇