Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya
Magharibi – Sospeter Magesse akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya
sh. Milioni 42.5 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu- Festo Kiswaga (kulia),
ikiwa ni mchango wa benki hiyo kwa ajili ya Maonyesho ya Nanenane
Kitaifa yatakayofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoani humo. (Katikati)
ni Katibu Tawala wa Mkoa – Mariam Mmbaga na Meneja wa NMB Tawi la NMB
Bariadi – Gabriel Paul.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya
Magharibi – Sospeter Magesse (kushoto) akimkabidhi Tisheti Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu – Festo Kiswaga (kulia), kama udhamini wa Benki hiyo
katika Maonyesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika viwanja vya
Nyakabindi Mkoani humo.
………………………………………………………………………………………….
Benki ya NMB imetoa Shilingi
Milioni 42,500,000 kwa ajili ya kudhamini maonyesho ya Nanenane ya
yatakayofanyika kitaifa Kanda ya Magharibi katika viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kwa
kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua
Viongozi Bora 2020“.
Pamoja na kiasi hicho cha
pesa, Benki hiyo imekabidhi T-shirt 300 zitakazotumika kwenye maonyesho
hayo, ikiwa ni moja ya udhamini wake. Huu ni mwaka wa tatu mfululizo
Benki ya NMB inadhamini Maonyesho hayo.
Akikabidhi mfano wa hundi ya Sh.
Mil 42.5 kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu Meneja wa benki hiyo Kanda ya
Magharibi- Sospeter Magesse alisema, Benki ya NMB kusaidia sekta ya
kilimo ni fahari kwao kwani kupitia kilimo benki imekuwa ikifanya
biashara kubwa ambayo imechangia kukua kwa sekta hiyo.
“Kwa miaka mitatu ambayo
maonesho hayo yamefanyika Mkoani Simiyu,tayari NMB tumetoa udhamini wa
zaidi ya Mil 100, hii ni katika kuhakiksha sekta hii inakuwa imara na
kuongeza pato la taifa,” alisema Magesse
“Katika kuunga mkono juhudi za
Rais wetu wa awamu ya tano,Dkt John Magufuli kwa miaka mitano ya awamu
ya tano ya serikali yake,mchango wetu kama benki tumeweza kujenga uchumi
imara kupitia kilimo na ufugaji” Magesse.
Aliongeza kuwa ndani ya miaka
miwili Benki hiyo imefanikiwa kufungua akaunti 500,000 za wakulima
ambapo kwa Mkoa wa Simiyu jumla za akaunti 86,000 za wakulima wa pamba
zimefunguliwa.
Meneja huyo alisema kuwa kama
Benki kinara nchini itaendelea na iko tayari kuendeleza uhusiano wenye
manufaa kati yao ,wakulima, wafugaji na wadau wengine wa kilimo ili
watumie fursa vizuri zilizopo kwenye soko na kukuza mitaji ya biashara
zao.
Akipokea mchango huo kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa huo – Antony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi- Festo
Kiswaga ameishukuru Benki hiyo kwa namna ambavyo wanajitoa kusaidia
maendeleo ya wananchi hususani wakulima ambao ndio chanzo kikuu cha
ukuwaji wa uchumi wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya
kilimo bora kwa wakulima, kuwapatia mikopo na kuwafungulia akaunti
wakulima.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇