LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2020

TAKUKURU PWANI YAFANIKISHA MWALIMU MSTAAFU KUREJESHEWA MILIONI 4.9 ZA 'MKOPO UMIZA'

Mwalimu mstaafu Yusuph Rashid Kimweri
Na Scolastica Msewa, Kibaha
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Pwani imefanikiwa kurejesha fedha taslimu sh. 4,900,000/- kwa Mwalimu mstaafu Yusuph Rashid Kimweri ambaye alimlipa Ibrahim Marema Maswe ikiwa ni marejesho ya mkopo unaojulikana mkopo umiza.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa ya kazi ya kila miezi mitatu ofisini kwake mjini kibaha Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani Suzana Raymond amesema Kupitia Ofisi ya TAKUKURU kituo maalum cha Chalinze  tuliweza kuokoa na kumrejeshea fedha Taslimu kiasi hicho cha fedha Mwalimu Mstaafu.

Amesema kupitia mkopo usiofuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamiwa na taasisi za fedha nchini maarufu kama mkopo umiza wa kiasi cha Shilingi 700,000/= aliokopa mwaka 2018 na kupitia riba deni kukua na kufikia Shilingi 13,000,000/= ambalo Mstaafu huyo alilipa mara baada ya kupokea pensheni yake ya kustaafu tarehe 27 mei 2020.

Suzana amesema TAKUKURU baada ya kupata malalamiko juu ya mkopo huo walifanya uchunguzi wa kina na kubaini kwamba mtuhumiwa alifanya biashara ya kukopesha fedha kinyume na kanuni ya 4 ya Microfinance Act ya Mwaka 2019.

Aidha baada ya mtuhumiwa kutambua kosa aliahidi kurejesha fedha hizo Mtuhumiwa ameanza kurejesha fedha hizo mpaka sasa amesharejesha kiasi cha Tshs. 4,900,000/-na mtuhumiwa bado anatakiwa kurejesha kiasi cha Shilingi 8,100,000/= kilichobaki.

Aidha Mwalimu huyo Mstaafu Yusuph Rashid Kimweri ameishukuru taasisi hiyo ya kupambana na rusha TAKUKURU kwa kazi nzuri wanazofanya kusaidia wanyonge.

TAKUKURU imeweza kuokoa Shilingi 35,000,000/= kati ya Shilingi 394,156,335.30 ambazo ni fedha za malipo ya korosho kwa wakulima mkoani Pwani.

Kwani kampuni ijulikanayo kama MAFUBILO GENERAL SUPPLIES LTD ya jijini Dar Es Salaam.

Ambayo ilinunua kwa mkopo korosho wa wakulima kupitia AMCOS za Visiga, Misugusugu, Kongowe, Mwendapole, Mkombozi na Miembe saba zenye jumla ya Shilingi 394,000 hivyo Malipo ya korosho hizo yalisuasua mpaka TAKUKURU ilipofanyia kazi na kuhakikisha mnunuzi analipa.

Na mdaiwa amepewa maagizo ya kulipa mpaka amalize deni lote haraka iwezekanavyo ili wakulima wapate haki yao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages