Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo Getruda Bonifasi Simiza.
Na Scolastica Msewa, Bagamoyo
Makada 55 Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza na kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Akizungumza ofisini kwake jana, Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo Getruda Bonifasi Simiza, amesema idadi hiyo ni hadi kufikia jana saa 10 jioni, Julai 15, 2020, ikiwa ni siku ya pili tangu mchakato wa uchukuaji fomu hizo ulipoanza juzi, Julai 14, 2020 ndani ya CCM.
Getruda amesema wilaya ya Bagamoyo ina majimbo ya uchaguzi mawili yaani jimbo la Bagamoyo na jimbo la Chalinze ambapo jimbo la Bagamoyo wana CCM 37 wamejitokeza kuchukua fomu na wanaCCM 18 wamejitokeza kuchukua fomu kugombea ubunge jimbo la Chalinze wakati kati yao ni watano wanawake.
Aidha katibu hiyo wa CCM wilaya ya Bagamoyo amewataka wote waliochukua fomu kugombea kuzingatia sheria na taratibu za Chama pamoja na taratibu na sheria za nchi kwani vyombo vya usalama vipo macho kuwafuatilia nyendo zao.
Your Ad Spot
Jul 16, 2020
Home
featured
siasa
MAKADA 55 WA CCM WAJITOKEZA HADI JANA KUCHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA BAGAMOYO
MAKADA 55 WA CCM WAJITOKEZA HADI JANA KUCHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA BAGAMOYO
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇