LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 22, 2020

RAIS MAGUFULI AZINDUA JENGO LA TAKUKURU CHAMWINO, DODOMA






   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua Jengo la Ofisi za TAKUKURU wilaya ya Chamwino akiwa  na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi wengine eneo la Chikuyu B Chamwino mkoani Dodoma leo Jumatano Julai 22, 2020

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Jengo la Ofisi za TAKUKURU wilaya ya Chamwino eneo la Chikuyu B Chamwino mkoani Dodoma leo Jumatano Julai 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wakati wa uzinduzi hafla ya  Jengo la Ofisi za TAKUKURU wilaya ya Chamwino eneo la Chikuyu B Chamwino mkoani Dodoma leo Jumatano Julai 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo wakati akikagua Jengo la Ofisi za TAKUKURU wilaya ya Chamwino eneo la Chikuyu B Chamwino mkoani Dodoma leo Jumatano Julai 22, 2020


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Julai, 2020 amezindua majengo 2 ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) yaliyopo Jijini Dodoma na Chamwino.

Jengo la NEC lenye ghorofa 8 limejengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la Suma-JKT katika eneo la Njedengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 12.3 baada ya kupokea kazi hiyo kutoka kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) waliokuwa wametumia shilingi Bilioni 4.2

Jengo la ofisi ya TAKUKURU Chamwino ambalo ni moja ya majengo 7 yaliyojengwa katika wilaya 7 hapa nchini, limejengwa kwa utaratibu wa ‘Force Account’ ambapo TAKUKURU imetumia shilingi Bilioni 1 sawa na takribani shilingi Milioni 143 kujenga kila ofisi kwa kutumia wataalamu wake yenyewe na majengo yote yamekamilika.

Akizungumza baada ya kuzindua jengo la NEC, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza NEC akianzia na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliyeokoa shilingi Bilioni 12 katika matumizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambazo zilielekezwa kujenga jengo hilo na Mwenyekiti wa sasa Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage  pamoja na Chuo Kikuu - Ardhi kwa kusimamia kwa karibu ujenzi wa ofisi hiyo ambayo ipo tayari kuanza kutoa huduma.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi wa vyama vya siasa walioshiriki katika uzinduzi wa jengo hilo, na ametoa wito kwao, viongozi wengine na Watanzania wote kwa ujumla kuendela kushirikiana katika ujenzi wa Taifa na kuhakikishia wanashiriki mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu bila kusababisha fujo, vurugu ama vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.

“Niwaombe viongozi wenzangu wa vyama vya siasa, uchaguzi huu uwe wa kipekee, tufanye kampeni zetu kwa upole, tufanye kampeni zetu kwa kumtanguliza Mungu, tufanye kampeni zetu kwa kujua sisi ni Taifa la Tanzania, tufanye kampeni zetu kwa kujenga umoja wa Taifa letu Tanzania, tunadi sera zetu na wananchi waweze kutupima kutokana na sera zetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wao viongozi wa vyama vya siasa wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi kubwa za ujenzi wa Taifa na wameahidi kufanya siasa za kistaarabu.

Mhe. Rais Magufuli ametoa wiki 2 kwa taasisi mbalimbali za Serikali ambazo zinadaiwa shilingi Bilioni 12 na Shirika la Ulinzi la Suma Guard kulipa fedha hizo baada ya Mkuu wa JKT Mej. Jen. Charles Mbuge kudai kutolipwa kwa madai hayo kunakwamisha shughuli za shirika hilo.

Akizungumza katika sherehe za kuzindua Ofisi ya TAKUKURU Chamwino, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Taasisi hiyo kwa juhudi kubwa za kukabiliana na rushwa, kuokoa mali za umma  zikiwemo fedha, mashamba, magari, majengo na viwanja.

Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa kwake na gharama kubwa zilizotumiwa na TAKUKURU kujenga nyumba 7 kwa shilingi Bilioni 1 sawa na wastani wa shilingi Milioni 143 kwa kila nyumba, kwani majengo yaliyojengwa yanathamani ndogo ikilinganishwa na fedha zinazotajwa kutumia.
Amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jen Mbungo kurekebisha dosari hizo na pia ameishangaa TAKUKURU kwa kutaka kujenga ofisi ya taasisi hiyo katika Wilaya ya Chato kwa kuwa tayari wilaya hiyo inalo jengo la TAKUKURU alilolikabidhi yeye mwenyewe akiwa Waziri wa Ujenzi.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itatoa shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi wa TAKUKURU lakini amekataa ombi la fedha zote shilingi Bilioni 1 ambazo taasisi hiyo imeomba kwa ajili ya kujenga uzio katika ofisi mpya 7zilizojengwa wilayani, na kwamba Serikali itatoa fedha zisizozidi shilingi Milioni 500.

Sherehe za uzinduzi wa majengo ya NEC na TAKUKURU hapa Dodoma zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. 

Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri, Makatibu Wakuu, viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Dini na viongozi wa Mkoa wa Dodoma.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
22 Julai, 2020

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages