Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Abdul Njaidi (kushoto), akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la mfuko huo katika Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye Viwanja vya Mwaalimu Nyerere leo Julai 2, 2020. Katikati ni Meseka Kadala, Afisa Uhusiano wa Mfuko huo.
Dar es Salaam, Tanzania
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema katika msimu huu wa maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam unatoa huduma kamili kama ambazo zinazopatikana kwenye ofisi zake kote nchini.
Akizungumza na kwenye banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam , Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi amesema kwa mantiki hiyo Mfuko umewaalika wanachama wa Mfuko na wananchi kwa ujumla kufika katika banda hilo ili kujipatia huduma na taarifa mbalimbali.
“Tunawakaribisha wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kutembeela banda letu kwani huduma zote za kiofisi ambazo zinapatikana kwenye ofisi zetu zilizoenea kote nchini zinapatikana hapa.” Alisema Bw. Abdul Njaidi.
Alitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na mwanachama kupata taarifa kuhusu Pensheni, Mafao, uhakiki, uwekezaji na taarifa za michango.
Katika hatua nyingine, Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Uendelezaji Bishara Tanzania (TANTRADE), Theresa Chilambo amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuyafungua rasmi maonesho hayo Ijumaa Julai 3, 2020.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Donald Maeda akimsikiliza mwanachama wa Mfuko aliyefika kwenye banda la PSSSF ili kupata taarifa za michango yake. PICHA ZAIDI../BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇