1.0 UTANGULIZI
Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Usajili wa Laini za Simu) za
mwaka 2020, yaani “The Electronic and Postal Communications (SIM Card
Registration) Regulations, 2020”, zimeainisha katika Kanuni ya 18 kuwa:-
18 (1) Mtu anayehitaji kumiliki na kutumia laini ya simu ataruhusiwa kusajili:-
(a) Kama ni mtu binafsi
i. Idadi ya laini moja kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa ajili
ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe mfupi pamoja na
matumizi ya data;
ii. Idadi ya laini zisizozidi nne kwa kila mtoa huduma za mawasiliano
kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na mashine; na
(b) Kama ni Kampuni au Taasisi
i. Idadi ya laini zisizozidi thelathini kwa kila mtoa huduma za
mawasiliano kwa ajili ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe
mfupi pamoja na matumizi ya data;
ii. Idadi ya laini zisizozidi hamsini kwa kila mtoa huduma za
mawasiliano kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na
mashine.
(2) Laini zilizosajiliwa kwa matumizi yaliyoainishwa kwenye Kanuni 18 (1) (a)
hazipaswi kutumiwa kwa kubadilishana (interchangebly).
(3) Bila kujali Kanuni ya 18 (1), Mtu binafsi, Kampuni au Taasisi inaweza
kuruhusiwa kusajili na kumiliki laini zaidi ya zilizoainishwa kwa kuomba na
kupata idhini kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni hizi, atakuwa ametenda
kosa la jinai.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu umma
kwamba zoezi la kuomba idhini ya umiliki wa laini za simu zaidi ya moja
katika mtandao mmoja linaendelea. Tunawashauri wamiliki wa laini za
mawasiliano ya simu kuendelea kuhakiki usajili wa laini zao zote
wanazomiliki.
2.0 KUTHIBITISHA IDADI YA LAINI ZILIZOSAJILIWA KUTUMIA
KITAMBULISHO CHA TAIFA (NIDA)
2.1 Kila mmiliki wa laini ya simu anatakiwa kupiga namba *106# na
kuangalia usajili wa laini anazomiliki na endapo atakuta namba
ambayo haitambui na imesajiliwa kwa kutumia namba ya
kitambulisho chake cha Taifa anashauriwa kuwasiliana na mtoa
huduma wake ili azifunge mara moja kuepusha matumizi mabaya na
kumsababishia usumbufu usiokuwa wa lazima utakaojitokeza.
2.2 Kwa wale ambao kwa sasa wanamiliki laini zaidi ya moja katika
mtandao mmoja, mwisho wa kuhakiki laini zao itakuwa tarehe 31
Julai 2020.
2.3 Utaratibu wa kuomba idhini ya kumiliki laini mpya za ziada katika
mtandao mmoja unaendelea na mteja anaweza kupata huduma hii
kupitia kwa wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa
kutumia njia za kielektroniki mtoa huduma atawasilisha maombi ya
mteja wake TCRA kwa idhini ya kusajili na kumiliki laini za ziada;
mteja atapokea majibu ya maombi yake ndani ya takribani dakika
tano.
3.0 URASIMISHAJI WA LAINI ULIZOTHIBITISHA
3.1 Urasimishaji wa laini za ziada kwa sasa unaweza kufanyika kwa
wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa kutumia njia
za kielektroniki ambapo mtoa huduma atawasilisha maombi yake ya
idhini ya kurasimisha laini za ziada TCRA na kupokea majibu ndani
ya takribani dakika tano; au
3.2 Kwa kupitia namba *106# ambapo wewe mwenyewe utaweza
kuomba idhini ya kurasimisha kutoka TCRA kupitia simu yako.
Huduma hii ya kurasimisha kwa njia ya simu yako itaanza kutumika
rasmi Agosti 1, 2020.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Jengo la Mawasiliano,
Kitalu Na. 20 Barabara ya Sam Nujoma,
S. L.P 474,
14414 DAR ES SALAAM
1 Julai, 2020
Your Ad Spot
Jul 1, 2020
Home
Unlabelled
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA ISO 9001:2015 CERTIFIED TAARIFA KWA UMMA UFAFANUZI JUU YA UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA KURASIMISHA UMILIKI WA LAINI ZA SIMU ZAIDI YA MOJA KATIKA MTANDAO MMOJA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA ISO 9001:2015 CERTIFIED TAARIFA KWA UMMA UFAFANUZI JUU YA UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA KURASIMISHA UMILIKI WA LAINI ZA SIMU ZAIDI YA MOJA KATIKA MTANDAO MMOJA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇