LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 1, 2020

DK MAGUFULI AWASHUKURU WALIOMDHAMINI, ASEMA ANA DENI KUBWA (+VIDEO)

 Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM, waliofika Makao Makuu ya chama hicho, Jijini Dodoma kuhushudia alipokuwa akirejesha fomu za udhamini wa kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya ya CCM kugombea Urais wa Tanzania Oktoba 2020. Katika mkutano alitumia fursa ya kuwashukuru wanachama wote waliomdhamini na kwamba ana deni kubwa kwao. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeries akikabidhi  kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli fomu za wanachama waliomdhamini wa mkoa huo. Picha zingine ni wenyeviti wa CCM wa mikoa wakikabidhi  fomu za udhamini kwa Mwenyekiti wa CCM,  Rais Magufuli ambaye alirejesha fomu za kuomba kugombea urais wa Tanzania kupitia cha chama hicho.Na Richard Mwaikenda, Dodoma.


 Na Richard Mwaikenda,Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Dk. John Magufuli amewashukuru sana wote waliojitokeza kumdhamini kwa kujaza fomu za kuomba kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020, kupitia chama hicho.

Shukrani hizo alizitoa mara baada ya kurejesha fomu Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma, ambapo kwa kitendo hicho cha kudhaminiwa na zaidi ya wanachama milioni moja wa Tanzania Bara na Visiwani, amesema kinamfanya awe na deni kubwa kwao.

Pia, Dk. Magufuli aliwapongeza Wenyeviti wa CCM wa mikoa yote 32 kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kufanikisha udhamini huo mkubwa, licha ya kupata lawama nyingi kwa waliojitokeza kudhamini lakini walikosa fursa hiyo.

Aliwaomba wanachama waliokuwa na nia hiyo, wasivunjike moyo bali udhamini huo wauweke kwenye kura endapo mikutano husika ya chama itampitisha kuwa mgombea urais wa Tanzania kupita chama hicho, ili akapambane na wagombea wa vyama vingine.

Pia aliwaomba wanachama wa vyama vingine wampigie kura wakati wa kinyang'anyiro hicho, ili awatumikie Watanzania kutimiza malengo waliyojiwekea pamoja na kukamilisha miradi mbalimbali waliyoianza katika Serikali ya Awmu ya Tano inayoongozwa na yeye, ikiwemo ya Reli ya Kisasa ya Mwendo Kasi (SGR), Mradi mkubwa wa umeme wa Mwalimu Nyerere Rufiji na miradi mingine mingi.

Kabla ya kurejesha fomu, lilifanyika tukio la wenyeviti wa mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani kukabidhi fomu za waliomdhamini kutoka katika mikoa hiyo. Pi wenyeviti wa Jumuiya za chama hicho; Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Umoja wa Wazazi Tanzania na Umoja wa Vijana (UVCCM), walikabidhi fomu za waliomdhamini Dk. Magufuli.



































 Baadhi ya wanahabari wakiwajibika wakati Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli akitoa shukrani kwa wanachama waliomdhamini


 Mwenyekiti wa CCM, Magufuli akiwa na viongozi wa chama hicho wakiwemo viongozi wa Jumuiya za chama hicho.
 Mwenyekiti wa CCM, Magufuli akiwa na wenyeviti wa CCM wa mikoa.


Baadhi ya mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja na Rais, Mwagufuli na viongozi wengine wa chama.


 Makatibu wa CCM wa mikoa wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Magufuli na viongozi wengine
Rais Magufuli akiwa  viongozi wa CCM Makao Makuu ya CCM Dodoma
Mwenyekiti wa CCM, Magufuli akiaga baada ya kumaliza kazi ya kurejesha fomu

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages