LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 30, 2020

WENGI WAFURAHIA MAGUFULI AKIREJESHA FOMU DODOMA (+VIDEO)



 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli akionesha fomu alipokuwa akirejesha kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Bashiru Ally Kakurwa, jijini Dododma leo  baada ya kudhaminiwa na zaidi ya wanachama  milioni moja nchini. Leo  Juni 30 ndiyo mwisho wa kukabidhi fomu hizo za kuomba  kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM,  Dk. Bashiru  (kulia) akimuonesha Mwenyekiti wa Chama, Rais John Magufuli sehemu ya kusaini kabla ya kukabidhi fomu hizo.  Wanachama 1,023, 911 wamejitokeza kumdhamini katika mikoa yote 32 nchini.
 Katibu Mkuu wa CCM, Dk.  Bashiru akionesha fomu alizozirejesha kwake Mwenyekiti wa chama hicho, Dk. Magufuli. Dk. Magufuli anaomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang'anyiro cha urais wa Tanzania.


Baadhi ya viongozi wa  CCM wakiwemo Wenyeviti wa CCM wa Mikoa na Makatibu wa Umoja wa Wanawake wa Mikoa pamoja na  wanachama wengine wa chama hicho, wakiwa wamesimama huku wakipiga makofi kushangilia kitendo cha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Magufuli kurejesha fomu za kuomba kugombea urais 2020.
 Baadhi ya wanachama wakishangilia baada ya Mwenyekiti kurejesha fomu



Mwenyekiti wa CCM, Dk. Magufuli akionesha kadi yake ya uanachama ambayo ameilipia hadi 2021. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages