LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 14, 2020

WATANZANIA 57 WALIOKUWA WAMEKWANA AFRIKA KUSINI KUTOKANA NA CORONA WAREJEA NCHINI


Mmoja wa Watanzania waliokuwa wamekwama Afrika Kusini kutokana na nchi hiyo kufunga mipaka yake kutokana na Corona, Sunderland the only one akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka nchini humo, leo. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini humo Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi 
AFRIKA KUSINI
Watanzania 57 waliokuwa wamekwama nchini Afrika Kusini kutokana na janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19 baada ya nchi hiyo kufunga mipaka yake hatimae wamerejea nchini.

Watanzania hao 57 waliokuwa wamekwama Nchini Afrika Kusini kwa takribani miezi mitatu baada ya uwepo wa zuio la kutoka nje (lockdown) wameondoka nchini humo kwa kutumia Shirika la ndege la Precission air kutokana na uratibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuhusisha Ubalozi wa Tanzania Nchini humo.

Wakizungumza kwa furaha katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo uliopo Afrika Kusini mmoja wa Watanzania hao aliyefahamika kwa jina la Sunderland the only one ameishukuru Serikali kupitia kwa Balozi wa Tanzania nchini humo Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kwa kuwa pamoja nao katika kipindi chote ambacho wamekuwa katika zuio Afrika Kusini.

Kundi jingine kama hilo la watanzania 38 waliokuwa wamekwama Nchini Misri nao wamefanikiwa kuondoka nchini humo kwa shirika la ndege la fly Egypt.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages