Jimbo la Mbinga mjini lililopo katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, lina jumla ya Kata 19, na ni miongoni mwa majimbo ambayo yamebahatika kupata Wabunge Vijana. Baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2015, Jimbo hilo lilipahatika kumpata Mbunge Kijana anayeelezewa kuwa ni mchapakazi mahiri.
Baada ya mbunge huyo Mh. Sixtus Mapunda kukaribia kuhitimisha miaka yake ya Ubunge katika jimbo hilo, yeye na timu yake wametayarisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM sambamba na utekelezaji wa ahadi za Ubunge huyo jimboni. Nasi kwa kutambua umuhimu wa Taarifa hiyo tumeichapisha ili Wana CCM na Watanzania wote kwa jumla muweze kuisoma na kuielewa vema.
Kwa ufupi katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi 2019/2020 yamefanyika mambo kamambe ambayo kwa mujibu wa Mheshimiwa Sixtus Mapunda anasema katika kipindi cha miaka mitano jumla ya sh. Bilioni kumi na tatu milioni Mia moja kumi na tatu, laki Saba sabini na Saba mia nane kumi na tano na senti themanini na moja (Sh. 13,113,777,815.81) zimetumika katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi za Mbunge na kwamba kati ya fedha hizo, Sh. 1,346,950,322/= zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri na Sh.151,715,200/= zimetoka kwenye mfuko wa Jimbo.
Mheshimiwa Sixtus anasema Sh. 9,740,608,578.81 zimetoka serikali kuu, Sh. 1,728,803,915/= zimetoka kwa wahisani, na Sh. 145,718,566.95 zimetoka kwa Mbunge huyo wa Mbinga mjini na marafiki zake ikiwa ni pamoja na Ubalozi wa China, NMB, TAWA na TUTUNZE.
Anasema , katika kipindi hicho chote cha miaka mitano, utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa namna moja au nyingine umefanyika kwa kata zote na kwamba hakuna Kata hata moja ambayo haijanufaika na jitihada za Serikali ya awamu ya Tano katika kusukuma mbele maendeleo kwa wananchi. Sasa kuisoma Taarifa hiyo hatua kwa hatua, Tafadhali>> BOFYA HAPA
Your Ad Spot
Jun 14, 2020
Home
featured
siasa
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM NA AHADI ZA MBUNGE WA MBINGA MJINI SIXTUS MAPUNDA 2015-2020
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM NA AHADI ZA MBUNGE WA MBINGA MJINI SIXTUS MAPUNDA 2015-2020
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇