Viongozi wa Marekani wamekosoa vikali uamuzi wa Rais Donald Trump wa kutuma wanajeshi kwa lengo la kukabiliana na waandamanaji.
Zaidi ya wanadiplomasia 280, majenerali na viongozi wa usalama wa taifa nchini Marekani Ijumaa walimtaka Trump kuacha kuwatumia vibaya wanajeshi kwa malengo ya kisiasa. Viongozi hao wa Marekani wametoa taarifa ya pamoja ya maandishi inayosema: "Utumiaji mbaya wa askari kwa malengo ya kisiasa, unadhoofisha muundo wa kidemokrasia wa Marekani." Taarifa hiyo pia imeeleza kwamba, kurusha angani helikopta katika umbali wa chini kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji, ni kutojali kama ambavyo hakuna ulazima.
Hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani alitishia kwamba iwapo magavana wa majimbo ya nchi hiyo hawatachukua hatua zinazofaa kwa ajili ya kukabiliana na waandamanaji, basi atatoa amri ya moja kwa moja kwa wanajeshi waingie mitaani. Hii ni katika hali ambayo, Mark Esper, Waziri wa Ulinzi wa Marekani siku ya Jumatano alipinga uamuzi wa Trump wa kulitumia jeshi kukandamiza maandamano ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇