Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Polisi kutoa taarifa kuhusu tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
Mbowe inadaiwa kuwa amevamiwa akiwa nyumbani kwake na kisha kushambuliwa na watu wasiojulikana ambao wamemjeruhi kwa kumvunja mguu.
Akizungumza mbele ya wabunge, Juni 9,2020, Spika Ndugai amesema ameenda kumjulia hali Mbowe akiwa katika kituo cha afya ambako alikwa amelazwa akipatiwa matibabu na kwamba kwa jinsi alivyumuona sio kama ambavyo inazungumza na baadhi ya watu.
"Niseme tu msichukulie kama hivyo mnavyochukulia, vyombo vya ulinzi na usalama vitoke mapema na viseme kimetokea nini, sio kazi yangu, wanachokijua wakisema wakati upelelezi unaendelea. Kesho muda kama huu tutakuwa na chakusema. Niwahakikishe Dodoma ni salama kabisa kabisa, mmekaa hapa tangu Aprili, hakuna aliyepoteza sikio, jicho wala aliyepoteza kidole, Dodoma ni salama,"amesema Spika Ndugai.
Akifafanua zaidi Spika Ndugai amesema kwa jinsi tukio hilo lilivyo anapata ugumu hata wa kulielezea lakini ameomba lisihusishwe na siasa kwani halina siasa ndani yake."Nilishindwa kueleza hili jambo lilivyo. Mtu aliyeumizwa anaweza kwenda kituo cha afya?Kweli?
"Hapa nina barua ya Halima Mdee kwamba wanaomba ndege wampeleke Dar es Salaam lakini wakati wanaomba ndege tayari wenyewe wameshakodi ndege. Waziri Mkuu ameenda kumuona, Rais amekwenda kumuona na tutaendelea kumsaidia. Tusiingize siasa kwenye jambo hilo,"amesema Spika Ndugai.
Kwa upande wake Mbunge wa Kilombero kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Peter Lijualikali amesema kuwa tukio la kushambuliwa kwa Mbowe ni mchezo tu ambao umepangwa."Tuko kwenye Corona wote tunajua, Chadema imekuwa ikifanya vitu vyake kitaalam kwa ajili ya kupambana na Corona. Hawataki kugusana kwa ajili ya Coronaa, Chama hiki hiki jana limetokea jambo.
"Jana mpaka saa tatu baadhi ya wabunge akiwemo Peter Msigwa na Godbless walikuwa kwa Mwenyekiti, ukweli unafahamika walikwenda kulewa, na spika niseme vizuri, Msigwa amenukuliwa anasema tangu saa moja uisiku walikuwa kwa Mwenyeiti, baadae wakaachana.
"Tunajua alienda kunywa, tunajua mheshimiwa Mbowe kapanda ngazi kateleza kaanguka, huu ni ukweli kabisa, ukimsikia Msigwa analalamikia Mbowe alinyimwa walinzi. Tundu Lisuu alishambuliwa na walisema ameshambuliwa na System. Leo wanalalamika walinzi wameondolewa kwa Mbowe. Ni uongo,"amesema Lijualikali.
Ameongeza kuwa leo wanalalamika Mbowe ameondolewa walinzi wake ambao ni wale wale System, huo ni uongo, na kwamba Chama hicho kwenye Corona, mchana wako Lock down usiku anakwenda kulewa.
"Chadema imekuwa ikilalamika , Chadema , inawezakana vipi kiongozi wa Bunge anatembea usiku tena saa saba usiku peke yake.Wanasema wao ni chama chenye umakini, ni umakini gani huo"Umakini upi huo.Umeshasema Lissu ameshambuliwa Dodoma, wewe kiongozi unatembea usiku peke yako. Hizi ndio wanasema akili mbadal, hii ndio akili mbadala.
"Kwenye vikao unasema tungeweza kukaa kimya lakini wameingiza siasa kwenye jambo hilo.Uvunjwe leo kwenye uchaguzi wa mwezi wa kumi, uvunjwe leo?Yaani miezi yote hii uvunjwe miguu leo?Watanzana naomba mfahamu, Mwenyekiti hii michezo inafanyika, ni usanii kwanini kaenda kituo cha afya binafsi alidhani atafichiwa siri"amesema Mbunge huyo.
Ameongeza wakati akiendelea kuzungumza hapo bungeni, Mbowe tayari ameshapanda ndege kwenda Dar es Salaam."Hivi kweli ukanyagwe unaweza kunyanyuka kweli. Mheshimiwa Rais Magufuli, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na wana-CCM nataka kuwaambia mko salama.
"Yanayofanywa na upinzani ni kupoteza muda. Huku ni sehemu ya kufanya dili zao,vijana wanadhani watu wanaimani ya kukomboa nchi, hiyo imani ambayo mnayo watu wanaitumia vibaya kupiga fedha. "Huyu mzee haumwi, huyu mzee hajapigwa, hajakanywa bali anazusha".
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇