Godfrey Chikandamwali
Na Bashir Nkoromo Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sinza kwa tiketi ya Chadema Godfrey Chikandamwali jana, alimaliza udiwani wake kwa kuwekwa 'rokapu' na Polisi na kisha kufunguliwa jalada TAKUKURU, kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori, kwa tuhuma za kukaidi wito wa mkuu huyo wa wilaya na pia kutafuna mamilioni ya fedha za kikundi cha kina mama.
Akizungumza kwenye Kikao cha mwisho cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Mkuu huyo wa Wilaya alimwagiza Mkuu wa Polisi katika Wilaya hiyo Godfrey Jengela kumkamata Diwani huyo na kumuweka 'rokapu' kwa sababu ya kukaidi wito wake na kisha apelekwe TAKUKURU ili kufunguliwa jalada la uchunguzi juu tuhuma za ulaji wa fedha za kikundi cha Millenium Women Group ambacho kilipewa fedha kama kikundi katika mwaka wa fedha 2016-17, na hizo fedha hadi sasa hazijulikani ziko wapi na hivyo kama itathibitika zililiwa kwa kufungua akaunti feki diwani huyo achukuliwe hatua za kisheria.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aloimwita ofisini kwake diwani huyo ili kuzungumza naye kuhusu mgogoro uliokwamisha kuridhiwa kwa Kamati ya Hospitali ya Sinza, ikielezwa kuwa sababu kubwa ni diwani huyo kuingiza masuala ya siasa katika jambo hilo muhimu linalohusu usimamizi wa afya za wananchi.
"Mkuu wa Wilaya miongoni mwa majukumu yake ni kusimamia sheria na taratibu mbalimbali, zikiwemo shughuli zote za seikali, na tunapozungumzia shughuli za serikali ni pamoja na shughuli zinazofanywa na Halmashauri, siyo jamani? kwamba shughuli zote za serikali zinazofanywa katika wilaya ikiwemo na yale yanayofanywa na Halmashauri yanafanywa kwa mujibu wa sheria, sera miongozo, kanuni na maelekezo mbalimbali ya viongozi wetu ili kueleta ustawi kwa jamii yetu kwa jumla.
Kwa hiyo kwa dirisha hilo nimefanya 'attempt' nimefanya jitihada za kujaribu 'rescue' hili suala la kamati, kwa sababu lazima tujenge haiba nzuri ya mtumishi, kama tutakuwa na utaratibu wa kwamba kila mtu anaendesha ofisi kama familia hatuwezi tukafika, hata familia kuna mipaka fulani fulani, hata mkeo kama unakikiuka mipaka fulani fulani anaweza kukupeleka hata mahakamani. Ikiwa hata familia kuna 'cotrol' ya kufanya mambo, sasa 'Generation' yetu hii ambayo tumepewa dhamana ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu mbele, lazima tuzingatie 'proffesionalism', Alisema Mkuu huyo wa Wilaya na kuongeza;
"Sasa jana nilimuomba Mstahiki Meya tuzungumze ofisini na Mheshimiwa Diwani wa Kata Sinza kuhusu hili suala hili, kwa sababu hatuwezi tukaendesha shughuli za serikali kwa 'mapembe' tu, lazima tujenge hoja tukubaliane, lakini hilo halikuwezekana, Mheshimiwa diwani hakufika ofisini, lakini leo pia nikamwelekeza Katibu Tawala kwamba hebu zungumza na Mheshimiwa Diwani kwa sababu wito wa Mkuu wa Wilaya ni wito halali, kwa hiyo unapokaidi wito wa Mkuu wa Wilaya eeh, ina 'implications' zake lakini Mheshimiwa Diwani hakutokea leo, sasa sijajua ni kwa nini, Kwa hiyo OCD baada ya kikao hiki kuisha na Mwenyekiti kufunga Baraza nakuagiza kumuweka ndani Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Sinza.
La pili, kuna kikundi kinaitwa Millenium Woman Group, Kamanda wa PCCB wilaya, baada ya utekelezaji wa agizo langu kwa OCD, OCD utamkabidhi Mheshimiwa Diwani kwa Kamanda wa PCCB ili kufungua jalada la uchunguzi juu ya ulaji wa fedha za kikundi hiki cha Millenium Women Group ambacho kilipewa fedha kama kikundi katika mwaka wa fedha 2016-17, na hizo fedha hadi sasa hazijulikani ziko wapi, kama itathibitika zililiwa kwa kufungua akaunti feki kama tunavyofahamu basi achukuliwe hatua."
Mapema Wakati Kikao hicho cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kikiendelea ulirejea tena mjadala kuhusu kuthibitishwa kwa Kamati ya Hospitali ya Sinza, ambao unaelezwa kuwa umekuwa ukiibuka kila Baraza linapokutana na kumalizika bila kupatikana ufumbuzi huku ikielezwa kuwa kikwazo huwa ni Diwani huyo wa Kata ya Sinza ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira wa Baraza hilo ambalo kikao chake cha jana kilikuwa cha mwisho.
Ili Kamati hiyo iweze kutambuliwa na kufanya kazi, ilipaswa ipitishwe na Baraza la Madiwani ili Mkurugenzi wa Manispaa aandike barua ya kuitambulisha kamati hiyo, Tawala za Mikoa na srikali za Mitaa (TAMISEMI), lakini hatua hiyo imekwama.
Inaelezwa kuwa Baraza limekuwa likikwama kupitishwa kwa Kamati hiyo kutokana na kuingizwa itikadi za kisiasa hivyo kwa kuwa Chadema ndiyo waliokuwa na Madiwani wengi katika Baraza hilo walikuwa wakikwamisha kura zinapopigwa kwa kuwa waliokuwa Wajumbe wa Kamati hiyo waliokuwa wanawataka hawamo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇