LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 12, 2020

RATIBA YA MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WA NAFASI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA RAIS WA ZANZIBAR KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020



RATIBA YA MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WA
CHAMA CHA MAPINDUZI WA NAFASI YA RAIS WA 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA RAIS
WA ZANZIBAR KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA 
MWAKA 2020


1.0.         URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

NA
TAREHE
SHUGHULI/MAELEZO

1
15 – 30/06/2020
Kuchukua na kurejesha fomu. Mwisho wakurudisha fomu ni tarehe 30/6/2020 Saa 10:00 jioni.

2
15 – 30/06/2020
Kutafuta wadhamini Mikoani.

VIKAO VYA UCHUJAJI
3
06 – 07/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
4
08/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Taifa.
5
09/07/2020
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
6
10/07/2020
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa: Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa majina yasiyozidi matatu ya wanachama wanaoomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7
11 - 12/07/2020
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



                                       2.0. URAIS WA ZANZIBAR
NA
TAREHE
SHUGHULI/MAELEZO
1
15 – 30/06/2020
Kuchukua na kurejesha fomu. Mwisho wakurudisha fomu ni tarehe 30/6/2020 Saa 10:00 jioni.
2
15 – 30/06/2020
Kutafuta wadhamini Mikoani.
VIKAO VYA UCHUJAJI
3
01 – 02/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.
4
03/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Zanzibar.
5
04/07/2020
Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kuhusu wanachama wanaoomba nafasi ya Rais wa Zanzibar.

6
09/07/2020
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watatu wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar.
7
10/07/2020
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea Urais Zanzibar. 
8
11 - 12/07/2020
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Kuthibitisha  jina la mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.






3.0.         MAMBO YA KUZINGATIWA NA KILA MGOMBEA
(i)            Kila mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa 
            Tanzania ni lazima apate wadhamini
                    250 katika Mikoa 12 angalau Mikoa 2 kati ya hiyo iwe
                    ya Zanzibar.

(ii)           Kila mgombea wa Urais wa Zanzibar ni lazima apate wadhamini
               250 katika Mikoa isiyopungua
              mitatu, kati ya hiyo angalau Mkoa mmoja kutoka Unguja na 
              mmoja kutoka Pemba.

(iii)          Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa hawaruhusiwi
               kumdhamini mgombea Urais
              wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(iv)         Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa hawaruhusiwi
              kumdhamini mgombea Urais wa Zanzibar.

(v)          Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea zaidi ya mmoja.

(vi)         Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa
             CCM wa Wilaya kwa kupigwa
              muhuri wa chama wa Wilaya husika.

(vii)         Wanachama watakaomdhamini mgombea, uanachama wao
              uthibitishwe na Katibu wa CCM wa
             Wilaya husika.

(viii)        Kila mgombea atalazimika kuzingatia maadili ya Chama 
              Cha Mapinduzi, masharti ya uongozi,
              sifa za wagombea na utaratibu wa kuomba uongozi kama
              ilivyofafanuliwa katika Kanuni za
             Uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya Dola, Kanuni
             za Uchaguzi na Kanuni Uongozi na Maadili.

 4.0         TAARIFA YA ZIADA
(i)             Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya Ubunge, 
                Uwakilishi na Udiwani wa Kata/Wadi
                na Viti Maalum kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
                watachukua na kurejesha fomu kati
                ya tarehe 14 na 17 mwezi Julai 2020. Mwisho wa kurudisha
               fomu ni tarehe 17/07/2020 Saa 10.00 jioni.

(ii)           Taarifa rasmi ya mchakato wa kuwapata wagombea wa 
                Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi za Ubunge,
               Uwakilishi na Udiwani wa Kata/Wadi na Viti Maalum kwa
               ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
               itatolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi tarehe 11/07/2020.
               


               MFULULIZO WA MATUKIO YA RATIBA YA
MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WA CHAMA
CHA MAPINDUZI WA NAFASI YA RAIS WA JAMHURI 
YA MUUNGANO WA TANZANIA NA RAIS WA ZANZIBAR
WA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020

MUDA/TAREHE
SHUGHULI/MAELEZO
15     – 30/06/2020
i)       Kuchukua fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar. 
ii)      Kutafuta wadhamini Mikoani.
iii)     Kurejesha fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar. Mwisho tarehe 30/6/2020 saa 10:00 jioni.
01 – 02/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.
03/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Zanzibar.
04/07/2020
Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kuhusu wanachama wanaoomba nafasi ya Rais wa Zanzibar.
06 – 07/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
08/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Taifa.
09/07/2020
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na majina ya wanachama wasiozidi watatu wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar.
10/07/2020
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea Urais wa Zanzibar na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa majina yasiyozidi matatu ya wanachama wanaoomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).
11 - 12/07/2020
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuthibitisha  jina  la mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.



2 comments:

  1. Ni Ratiba nzuri inayowapa fursa ya kugombea ubunge au Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi wale ambao hawakubahatika kuteuliwa kugombea Urais.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages