LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 28, 2020

RAIS DK. MAGUFULI AMTUMBUA HADHARANI ALIYEKUWA DAS WA KISARAWE MTELA MWAMPAMBA, AMTEUA MWANANA MSUMI PAPO HAPO KUCHUKUA NAFASI, LEO

Rais Dk. Magufuli akizungumza alipozindua Mradi mkubwa wa maji, Wilayni Kisarawe mkoa wa Pwani, leo, ambapo alitangaza pia kutengua uteuzi wa aliyekuwa DAS wa wilaya hiyo Mtela Mwampamba na kumteua papo hapo aliyekuwa Afisa Tawala wa Kisarawe Mwanana Msumi kushika nafasi.

CCM Blog, Kisarawe
Rais Dk. John Magufuli amemtumbua hadharani aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe (DAS ), Mtela Mwampamba na kumteua muda huo huo aliyekuwa Afisa Tawala wa Wilaya hiyo Mwanana Msumi kuchukua nafasi hiyo, wakati akizindua mradi wa maji wilayani humo katika Mkoa wa Pwani, leo Juni 28, 2020.


“Lakini pia hapa kuna tatizo moja, la mteule wangu mmoja DAS, nimeambiwa ana mambo ambayo hayaendani na maadili ya kazi yake, kwamba anachukua hata wake za watu. nilikwishamuonya siku za nyuma, nafikiri hakuweza kuonyeka.

“Na kwa sababu jukumu langu ni pamoja na kusimamia maadili na nidhamu za watendaji, ninakuagiza mheshimiwa Jafo (Suleiman Jafo – Waziri wa TAMISEMI) uongee na mheshimiwa Mkuchika (George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora) kwamba huyu kazi ya U-DAS nimeitengua leo,” akasema Rais Magufuli.

Baada ya kutengua uteuzi Rais Magufuli akaagiza Mwampamba atafutiwe kazi ya chini inayoendana na uwezo wake, lakini pia kazi hiyo asifanye ndani ya Wilaya ya Kisarawe.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages