LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 19, 2020

NDUGU ZAKE FLOYD WAISHIKA MIGUU UN, WAIOMBA IWASAIDIE WAMAREKANI WEUS

  • Philonise Floyd
Nduge zake George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa kikatili na polisi mzungu huko Marekani, wameuomba Umoja wa Mataifa kuwasaidia watu weusi wa Marekani na kusikiliza kilio chao.
Philonise Floyd ambaye ni ndugu yake George Floyd jana alihutubia kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Geneva huko Uswisi kujadili ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi ya Marekani dhidi ya raia weusi, akitoa wito wa kuundwa tume huru ya kufanya uchunguzi kuhusu ukatili wa polisi ya Marekani dhidi ya watu weusi. 
Philonise Floyd amewaambia wajumbe wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa katika mkutano huo ulioitishwa na nchi za Kiafrika kwamba: "Nyinyi mnao uwezo wa kutusaidia sisi Wamarekani weusi ili tufanyiwe haki na uadilifu."
Philonise ameashiria mauaji yaliyofanywa na polisi mzungu dhidi ya ndugu yake, George Floyd, katika mji wa Mineapolis nchini Marekani na akasema: Mbinu iliyotumiwa na polisi kumtesa na kumuua kaka yangu tena mbele ya kamera ndio mwenendo wa siku zote wa polisi ya Marekani dhidi ya raia weusi wenye asili ya Afrika. 
Philonise Floyd
Nchi 54 za Kiafrika zimelitaka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kushughulikia suala la ubaguzi wa rangi unaofanywa na polisi ya Marekani na mienendo ya kikatili dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika. 
Ilitazamiwa kuwa, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lingetayarisha muswada wa kuundwa kamisheni ya uchunguzi kuhusu ubaguzi wa rangi wa kimfumo na sulubu zinazowapata Wamarekani wenye asili ya Afrika. 
Maandamano ya kupinga ukatili na mauaji ya Wamarekani weusi
Hatua hii imechukuliwa baada ya polisi mzungu kumuua kikatili Mmarekani mweusi, George Floyd katika mji wa Mineapolis tarehe 24 mwezi uliopita.  

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages