LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 10, 2020

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. GODWIN MOLLEL ATETA NA MADEREVA WA MALORI NAMANGA

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto zinazowakumba.

Dkt. Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi kuwa itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga.

“Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa ” alisema.

Aidha, Dkt. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho, Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwapa salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na kusema anawapenda sana.

Mbali na hayo Dkt. Mollel alisema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika mpaka wa Namanga ni suala mtambuka ambalo linahusisha Wizara zaidi ya moja, huku akiweka wazi kuwa suala hili lina uhusiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo.

Nae, dereva wa malori yanayokwenda nchini Kenya Bw. Abdullah Hassan amesema kuwa, kama madereva hawakubaliani na majibu ya vipimo wanavyopewa kutoka Kenya kutokana na vipimo hivyo kuonesha idadi kubwa ya madereva kuwa na ugonjwa wa Corona jambo ambalo sio kweli.

“Tunaishi maisha magumu sana kutokana na hali iliyojitokeza, na kunachosikitisha zaidi, sisi hatukubaliani na vipimo ambavyo tunapimwa upande wa pili.

Kwa upande wake, Japhet Jeremiah alisema kuwa, wamekuwa wakiombwa kiasi cha shilingi 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana Corona, hali aliyeweka wazi kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania.

“Sisi kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tumeambiwa tuna Corona, na mimi wiki mbili nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina Corona na sijawai tumia dawa yoyote mpaka sasahivi” alisema

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages