Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, akizungumza na wananchi wa kata hiyo wakati akiwashukuru na kuwaaga baada ya kuwatumikia kwa miaka mitano katika uongozi wake katika Uwanja wa Swala uliopo Tuamoyo Dar es Salaam. (Picha zote na Jumanne Gude).
TUSIMAME kwa dakika moja kumuombea Dua njema Rais wetu Dk. John Magufuli, pia wananchi tumpe tena kura nyingi katika uchaguzi unaokuja maana ametuongoza vizuri” alisema Diwani wa Kata ya Kigamboni Dotto Msawa.
Ombi hilo alilitoa Juni 9, 2020. Diwani huyo wakati akiwaaga na kuwashukuru wananchi wa Kata ya Kigamboni, baada ya kumaliza muda wake wa uongozi.
Alisema wananchi lazima tumuombee rais wetu kwakua amefanya mambo mengi mazuri hata yeye diwani amefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo na Ilani ya CCM kutokana na uongozi bora wa Dk. Magufuli.
Dotto alisema kufanikiwa kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa barabara, sekta ya afya, elimu, ajira na michezo ni kutokana na mchango wake mkubwa kutoka kwa rais hata yeye ilimpa kazi nyepesi ya kutekeleza Ilani ya CCM.
Alisema alipokuja kuwaomba kura aliwahaidi kusimamia sekta ya afya hususani huduma ya mama na mtoto na kuhakikisha kinamama wanajifungua sehemu salama.
Alisema serikali kuu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachongozwa na Rais Dk. Magufuli ilitoa fedha za kujenga vituo vya afya kila kata na sasa kituo cha Kigamboni kimekuwa bora na cha mfano katika vituo vyote.
Dotto alisema kwa upande wa elimu ameweza kufanikiwa kujenga Sekondari katika kata hiyo baada ya kuomba msaada mkubwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, paul Makonda.
Pia alisema barabara nyingi za kata hiyo zimejengwa kiwango cha lami na kiwango cha changarawe na nyingine zinaendelea kujengwa na wakandarasi wako kazini ambapo zitakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema kwa upande wa vijana amefanikiwa kuwatafutia ajira vijana zaidi ya 75 sehemu mbalimbali, lakini kati ya hao wengine 25 waliacha kazi wenyewe na wengine wanaendelea na kazi.
“Kwa uwezo wangu mdogo vijana zaidi ya 75 nimewatafutia ajira katika makampuni ya mafuta, makampuni ya gesi, madereva sekta ya ulinzi na hata wengine kwenye pantoni (kivuko), nilifanya hivyo kutokana na kuwajali vijana na kutokana na nafasi yangu ya udiwani, pia leo (jana) nawaaga ndugu zangu kwani 2015 nilipiga hodi mkanikaribisha na sasa nawaaga”, alisema.
Kwa upande wa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kigamboni, Nobert Nestory, alisema katika sekta ya elimu kata hiyo ina shule nne za serikali na wakati Rais Dk. John Magufuli anaingia madarakani na msaidizi wake Diwani Dotto Msawa, kata imefanikiwa kupeleka wanafunzi wa sekondali 508 kwa maana kidato cha kwanza kutoka shule za msingi.
Alisema viongozi wa kata wakiongozwa na diwani Dotto, walipambana kupata eneo la kujenga shule ya sekondali yenye hadhi ya ghorofa kufanya kuimalika kwa maendeleo ya elimu katika kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, akiwabidhi jezi na mipira kwa viongozi wa timu ya Kigamboni Veterani Fc, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake wakati akiingia madarakani kuinua sekta ya michezo.
Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, akiwabidhi jezi na mipira kwa viongozi wa timu ya Kula Tule Fc, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake wakati akiingia madarakani kuinua sekta ya michezo.
Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, akiwabidhi bao wachezaji wa mchezo wa bao baada kuwahidi wakati akiingia madarakani ikiwa ni kuinua sekta ya michezo.
Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, akiwa na viongozi wa CCM Kata na serikali baada ya kumaliza mkutano wa kuwashukuru na kuwaaga wananchi wa kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, akionyesha cheti cha shukrani na pongezi kutoka Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Kivukoni, baada kumaliza muda wake wa kuongoza kata hiyo. kushoto ni Hajji Simba katibu wa hamasa kata ya kigamboni na kulia ni katibu wa uvccm kata.
Msanii Zaibu Machupa akitumbuiza nyimbo mara baada ya Diwani wa kata hiyo Dotto Msawa, wakati akiwashukuru na kuwaaga baada ya kuwatumikia kwa miaka mitano katika uongozi wake, Dar es Salaam
Kigambini bado tunamuhitaji, Kigamboni bado tunampenda kwani kunamakubwa ambayo tunatarajia Mh, Diwani ayamalizie, tunamuomba aweze kutetea cheo chake wakati ukifika ili aiweke kata yake ya Kigamboni iwe mfano kwa barabara za ndani zipitike kwa urahisi na kwa kiwango cha lami na tunamuombea kwa Mungu Ishaallah Mwenyezi Mungu azidi kumbariki kwa moyo wake wa Upendo, Huruma, Utu wake, Uthamini wake kwa kila Rika.
Tunamuombea sana aweze kurudi madarakani wakati ukifika na pia tunaomba wana CCM wampokee na wampe ushindi wa kishindo ili awe mgombea kupitia tiketi ya CCM apeperushe bendera anatosha, kwani mpaka sasa usafiri wa kuelekea mikoani si lazima ukapandiee Ubungo.
Hayo yamesemwa na katibu wa uvccm wa kata hiyo, Naina ibrahim wakati akizungumza na mwandishi wa ahabari ambapo alisema; Usafiri wa mikoani unaweza ukaanzia katika Kata ya Mh, Diwani aliyemaliza muda wake aliyefanya vizuri katika kipindi chake ndani ya miaka mitano.
Your Ad Spot
Jun 10, 2020
DIWANI AMUOMBEA DUA NJEMA NA KUMUOMBEA KURA RAIS DKT. MAGUFULI
Tags
featured#
habari picha#
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
habari picha
Tags
featured,
habari picha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇