LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 1, 2020

TANZIA: WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA BALOZI DK. MAHIGA AFARIKI DUNIA, RAIS DK. MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk. Augustine Philip Mahiga amefariki dunia baada ya kuugua ghafla nyumbabani kwake jijini Dodoma.


Akitangaza kifo hicho, Rais Dk. John Magufuli amesema Balozi Dk. Mahiga amefariki leo alfajiri na kwamba alifikishwa Hospitali akiwa meshafariki dunia.

Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu, Spika wa Bunge Job Yustino Ndugai, Wabunge, Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria na wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuondokewa na mpendwa wao, na amesema anaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Amemuelezea Marehemu Balozi Mahiga kuwa alikuwa mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na Mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika njanya za Kimataifa kwa miaka mingi.

“Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililomtuma” amesema Rais Magufuli.

Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages