CCM, Lumumba
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaunga mkono mazungumzo yanayoendelea katika nyanja za kimataifa kuhakikisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Saharawi inapata Uhuru kwa sababu vita vina gharama kubwa ikiwa ni pamoja na kuua watu wasio na hatia
Kimebainisha kuwa wakati wote kimekuwa kikisimamia Haki na Usawa kwa Imani yake kwamba Binadamu wote ni sawa.
Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali mstaafu Ngemela Lubinga wakati akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Saharawi Mahayub Buyema Mahafudi katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Kanali mstaafu Ngemela Lubinga amemshukuru Balozi huyo kwa kufika ofisi za Chama Cha Mapinduzi na kumuahidi kwamba Msimamo wa Chama Chama Cha Mapinduzi dhidi ya Ukandamizaji na unyonyaji wa aina yoyote ni ule ule tangu enzi za TANU na ASP
Amesema kwamba kinachoendelea Tanzania baada ya Uhuru wake Mwaka 1961 ni Mapambano ya Kujikomboa Kiuchumi
Balozi huyo Mahayub Buyema ambaye alifika kwa lengo la kudumisha undugu uliopo kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Polisario Front amesema amefurahishwa sana na mwenendo wa Chama Cha Mapinduzi namna kinavyofanya siasa safi na yenye Maendeleo.
“Ninafurahi kufika hapa CCM Lumumba nikitambua kwamba Chama Vha Mapinduzi kimekuwa kimbilio kubwa kwa Vyama vya Ukombozi Barani Afrika “alisema Balozi Mahafud
Balozi Mahafud amefafanua kwamba Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere Aliiongoza Tanzania ambayo wananchi wake Walijitoa kwa hali na mali kuhakikisha vyama vilivyokuwa vikipigania Uhuru katika nchi zao vinafanikiwa.
Your Ad Spot
May 1, 2020
Home
featured
siasa
NGEMELA: CCM INAUNGA MKONO MAZUNGUMZO KUHAKIKISHA SAHARAWI INAPATA UHURU BILA VITA
NGEMELA: CCM INAUNGA MKONO MAZUNGUMZO KUHAKIKISHA SAHARAWI INAPATA UHURU BILA VITA
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇