LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 8, 2020

SERIKALI YAMWAGA AJIRA KKWA MADAKTARI 610


Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewataka Madaktari wapya 610 ambao wameajiriwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi walivyopangiwa kuanzia Mei 11 hadi 25 Mwaka huu wakiwa na nyaraka zao zote muhimu.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo wakati akitangaza ajira hizo za madaktari kwa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati nchini.

Tangazo la ajira za madaktari hao zilitolewa Machi mwaka huu ambayo mchakato wa kuwapata ulifanyika hadi Aprili mwaka huu kwa kuzingatia vigezo mbalimbali katika kupata madaktari mahiri.

Akizungumza na wandishi wa habari Waziri Jafo amewaagizaWakurugenzi wote nchini ambao madaktari hao wamepangiwa kwenye halmashauri zao kuhakikisha wanawaandalia posho za kujikimu punde tu watakaporipoti bila kuwacheleweshea.

Jafo amewataka pia Wakurugenzi hao kutowabadilishia vituo vya kazi madaktari hao kwa kuwapeleka katika vituo wanavyovitaka wao.

" Niwatake Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuzingatia maelekezo haya, wasiwabadilishie madaktari hawa vituo ambavyo washapangiwa. Siyo Daktari amepangiwa Hospitali ya Wilaya Mkurugenzi anamhamishia kwenye Kituo cha Afya.

Niwasihi madaktari ambao wamepata ajira hizi kufanya kazi kwa weledi mkubwa wakijua kwamba wameaminiwa kuwahudumia wananchi. Siyo wanachukua posho na mshahara halafu wanaanza kuleta visingizio vya kuacha kazi," Amesema Jafo.

Jafo amemshukuru Rais Magufuli kwa namna ambavyo ameiboresha sekta ya afya kwa kugawa ajira nyingi ndani ya muda mchache sambamba na kujenga vituo vingi vya Afya pamoja na Zahanati.

" Ajira hizi 610 zimeifanya sasa orodha ya madaktari ambao wameajiriwa kwenye miaka minne ya Serikali ya Rais Magufuli kufikia 9839 na hii ni kwa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati ambazo hizi zinasimamiwa na Wizara yangu," Amesema Jafo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages