Ni dhahiri kwamba kwa muda mrefu tumekuwa tukiangalia Parachichi kama zao la kawaida hasa katika nchi yetu ya Tanzania. Kwa sasa zao hili limekuwa kati ya mazao makuu ya biashara kutoka Tanzania.
Ni Kweli kwamba zao hili linalopatikana kwa wingi Njombe, Iringa, Mbeya na Kilimanjaro lenye asili ya muda mrefu kutoka Guatemala Mexico sasa limekuwa kati ya mazao makubwa ya biashara duniani. Zao hili kwa sasa linaipatia nchi ya Tanzania takribani Shilingi Bilioni 27.6 kwa Mwaka ikiwa ni kutoka Sifuri kwa miaka mitano iliyopita, Ni kweli kwamba chini ya miaka kumi iliyopita uuzaji wa bidhaa hii katika soko la kimataifa kutoka Tanzania halikuwahi kuwepo.
Kwa takwimu Rasmi kabisa kutoka taasisi ya TAHA inaonyesha kwa sasa Tanzania inauza zaidi ya Tani 9000 ya maparachichi katika soko la kimataifa. Na kwa bei ya mashambani imeonyesha kuongezeka kutoka shilingi 450 kwa kilo mwaka 2014 mpaka kufikia Shilingi 1500 mwaka 2020.Taasisi ya TAHA inaonyesha kufikia sasa Tanzania ina zaidi ya wakulima 10000 wanaojihusisha na kilimo cha bidhaa hii. Na hali hii imesababisha kuongezeka kwa usafirishaji wa nje kwa asilimia 380 ndani ya miaka mitano.
Soko kubwa la bidhaa hii linapatikana hasa katika mataifa mengi ya ulaya, Kwani bara la ulaya linanunua zaidi ya tani milioni moja ya Maparachichi kwa mwaka Na taasisi inayojihusisha na zao hili duniani (WAO) imekadiria kuongezeka kwa uhitaji kwa asilimia 50 zaidi katika miaka kumi mbele. Mataifa ya Ufaransa, Uingereza na Uholanzi ni kati ya mataifa yanayonunua zaidi bidhaa hizi kutoka Tanzania.
Kwa takwimu za mwaka 2018 zilionyesha bara la ulaya pekee lilikuwa linajumuisha asilimia 85 ya soko la maparachichi kutoka Tanzania. Nchi ya Tanzania ni mzalishaji mkubwa wa pili Afrika wa zao la parachichi Nyuma ya Ndugu zetu Kenya, Tukiwa na uzalishaji wa tani 190000 kwa mwaka na huku tani 5000 mpaka 10000 zikiuzwa katika soko la kimataifa.
Hata hivyo serikali ya Tanznaia imekuwa kipaumbele katika kutafuta masoko kwa ajili ya wakulima wa bidhaa.Wizara ya kilimo imekuwa kupaumbele katika kutafuta fursa ya kuweza kusafirisha bidhaa ya maparachichi katika soko la Uchina. Kwani soko hili linanunua bidhaa za dola za kimarekani milioni 108 kwa mwaka hii ikiwa inaonyesha ni soko la uhakika kwa wakulima wa Tanzania.
Ni vyema sasa kwa wakulima wengi ambao ni wadogo na wakati kuweza kuona Fursa hii na kuongeza uzalishaji. Na kutambua jamii ya maparachichi yanayohitajika katika soko la kimataifa hasa maparachichi jamii ya HASS. Lakini jamii ya FUERTE na maparachichi yetu asilia yamekuwa kati ya maparachichi yenye soko kubwa kimataifa. KILIMO NI AJIRA, FURSA ZINAFUNGUKA, WEKEZA.
info@malembofarm.ccom
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇