FĂ©licien Kabuga, miongoni mwa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, amekamatwa karibu na mji wa Paris, wizara ya sheria ya Ufaransa imetangaza.
Bwana Kabuga ameshikiliwa na polisi mjini Asnières-Sur-Seine, eneo ambalo alikuwa anaishi kwa utambulisho wa uongo.
Mahakama ya kimataifa ya mauji ya kimbari yaliyotokea Rwanda yamemshtaki bwana Kabuga mwenye umri wa miaka 84-kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa wahutu ambao waliuwa watu 800,000 mwaka 1994.
Walikuwa wanawalenga kundi dogo la jamii ya Tutsi pamoja na wapinzani wao siasa.
Marekani ilitoa dau la dola milioni 5 kwa atakayeweza kutoa taarifa kuhusu bwana Kabuga ili aweze kukamatwa.
Mwendeshaji mkuu wa mashtaka wa kitengo cha mahakama ya Umoja Wa mataifa kwa ajili ya Rwanda-'International Residual Mechanism for Criminal Tribunals' (IRMCT) mjini Hague - mahakama inayosikiliza kesi za uhalifu wa vita za Rwanda na iliyokuwa Yugoslavia - alisema polisi wa Ufaransa walimkamata bwana Kabuga siku ya Jumamosi, baada ya matokeo ya operesheni ya pamoja ya uchunguzi wa muda.
"Kukamatwa kwa bwana FĂ©licien Kabuga leo hii inatukumbusha wale ambao walihusika katika mauaji ya kimbari kuwa wanapaswa kuwajibishwa hata kama ni baada ya miaka 26 baava ya uhalifu waliotenda," Serge Brammertz alisema katika taarifa yake.
"Katika sheria za kimataifa, kukamatwa kwa Kabuga kunaonyesha kuwa tunaweza kufanikiwa kama tunakuwa na msaada ya kimataifa kukabiliana na hilo," aliongeza.
Bwana Brammertz ameelezea shukrani zake kwa Ufaransa , lakini alisema hatua hii imefikiwa kwa mchango uliotolewa na Rwanda, Ubelgiji , Uimngereza, Ujerumani, Netherland, Austria, Luxembourg, Switzerland, Marekani, Europol pamoja na Interpol.
Kufuatia taratibu ambazo ziko chini ya sheria ya Ufaransa, hukumu ya bwana Kabuga inatarajiwa kuhamishwa kwenda kitengo cha mahakama ya Umoja Wa mataifa kwa ajili ya Rwanda IRMCT, eneo ambalo kesi yake itasikilizwa.
Mwaka 1997, Bwana Kabuga alitajwa katika mahakama ya kimbari mara saba , kuhusika na mauaji ya kimbari , kwa kusuka mipango, kuua, kutishia kuua wakati wa kimbari.
Marekani ilisema bwana Kabuga alikuwa miongoni mwa waasisi na mwenyekiti wa chama cha Fonds de DĂ©fense Nationale (FDN), ingawa anadaiwa kutoa ufadhili kwa serikali ya Rwanda katika utekelezaji wa mauaji ya kimbari mwaka 1994 .
Alidaiwa pia kutoa msaada wa vifaa kwa wanamgambo waliofanya mauaji hayo kwa kuwapa silaha na sare na kuwapatia usafiri.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇