Serikali ya Italia imeweka saini amri itakayoruhusu usafiri wa kuingia na kutoka nchini humo kuanzia Juni 3, inapojiandaa kulegeza marufuku ya kutotoka nje iliyowekwa kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona.
Taifa hilo pia litaruhusu usafiri kati ya maeneo - ambayo kulikuwa kumedhibitiwa kuanzia siku hiyo.
Uamuzi huo unaashiria hatua kubwa katika juhudi za nchi hiyo kufungua tena uchumi wake baada ya zaidi ya miezi miwili ya kufungwa.
Italia ina moja ya viwango vya juu zaidi vya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa corona ulimwenguni, lakini kiwango cha maambukizo kimepungua katika siku za hivi karibuni.
Zaidi ya watu 31,600 walifariki katokana na virus vya corona nichini humo, idadi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nyuma ya Marekani na Uingereza.
Italia ilikuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kuweka marufuku ya kutotoka nje baada ya visa vya maambukizi ya corona viliporipotiwa katika eneo la kaskazini mwezi Februari.
Lakini kulegeza kwa sheria hizo kulianza mapema mwezi huu, iliporuhusu kufunguliwa tena kwa viwanda na bustani Mei 4.
Amri ya hivi punde ya kulegeza marufuku zaidi imetiwa saini na Waziri Mkuu Giuseppe Conte na kuchapishwa katika gazette rasmi la serikali mapema Jumamosi.
Baadhi ya maeneo nchini Italia yalikuwa yameomba kupunguziwa masharti, lakini Waziri Mkuu Conte alisema masharti hayo yataondolewa polepole ili kuzuia wimbi la pili la visa vya maambuzo.
Maduka na migahawa pia yanatarajiwa kufunguliwa kuanzia Mei 18 lakini watu watatakiwa kuzingatia amri itakayowekwa ya watu kutokaribiana.
Makanisa ya Kikatoliki yanajiandaa kurejea ibada siku hiyo, lakini kutakuwa na muongozo maalum wa kudhibiti maambukizi ya virusi ambapo waumini watatakiwa kufuata ikiwa ni pamoja na kuvalia barakoa.
Makundi engine ya kidini pia yataruhusiwa kuendesha ibada zao.
Taarifa zingine zinazojiri kimataifa:
- Nchi note barani Ulaya zimeendelea kuripoti ya kupungua kwa idadi ya vifo vya kila siku, marufuku ya kutotoka nje ikianza kulegezwa. Ureno na Uhispania nimiongoni mwa nchi zilizopunguza makali ya hatua za kukabiliana na corona.
- Uchumi wa Ujerumani - ambao ndio mkubwa zaidi Ulaya - umeripotiwa kupungua kwa 2.2% katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu, kutokana na hatari za janga la corona.
- Nelson Teich amekuwa waziri wa pili wa afya kujiuzulu ndani ya mwezi mmoja,baada ya kutofautiana na rais Jair Bolsonaro kuhusu jinsi serikali inavyoshughulikia mlipuko wa virusi vya corona
- Rais Donald Trump ameahidi kwamba Marekani itarejelea shughuli zake "kuwe chanjo ama kusiwe na chanjo ". Ametangazo mkakati wa kupatikana kwa change ya corona kufikia mwisho wa mwaka
- Viwango vya maambukizo nchini Uingereza vimependa na sasa ipo katika hatua ambapo virusi vimeanza kusambaa kwa haraka, serikali inasema
- Zaidi ya visa millioni 4.5 vya corona vimeripotiwa note duniani,kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins - Carib thuluthi mojo ya wagonjwa walioambukizwa virusi wamepona.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇