LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 11, 2020

HATA HUKU NCHINI UINGEREZA TUNAPIGA NYUNGU SANA TU-DK.ASHA-ROSE MIGIRO


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

BALOZI wa Tanzania nchini Uingereza Dk.Asha-Rose Migiro amesema katika kukabiliana na virusi vya Corona hata huko waliko nako wanapiga Nyungu(kujifukiza) kama kawaida maana kila mtu anatafuta namna ya kujiokoa.

Dk.Migiro amesema hayo leo Mei 11 mwaka 2020 na kufafanua licha ya kwamba yeye na Watanzania wengine kuwepo Uingireza  ukweli wanatambua nyungu ni kitu cha asili na huko  wanapiga nyungu sana tu."Unajua kila mtu anatafuta njia mbalimbali za kujiokoa."

Akifafanua zaidi wakati anahojiwa na kipindi cha 360 kilichorushwa na Clouds Media,Balozi Dk.Migiro amesema pia anatambua jitihada mbalimbali ambazo zinafanywa na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika kutafuta dawa ya kukabiliana na Corona.

"Kuna hatua ambazo zinaendelea kwa nchi za Afrika, kama ambavyo tunafahamu kwa sasa Corona haina dawa wa kinga, hivyo kila nchi inajaribu kuangalia namna ya kusaidia wananchi wenye kwenye janga hili.Hata dawa ya Madagasca napongeza Rais Dk.John Magufuli alivyoamua kutuma ndege kwa ajili ya kuifuata dawa hiyo.

"Tunafahamu mataifa yote yanahaha kutafuta dawa na hadi sasa hakuna dawa ambayo imethibika kisayansi kuwa inatibu Corona, hivyo dawa ambayo itapatikana kwa sasa basi hiyo hiyo itatumika, maana hata unapozuia watu wasinywe, kuna tiba ipi nyingine mbadaka ambayo unampa atumie.Hivyo dawa ambayo imetolewa na Madagasca kwa Tanzania ni hatua nzuri.

"Na nimeona kupitia mitandao kwetu hapo nyumbani Tanzania kuna jitihada ambazo zinafanyika kupata dawa na nimeona kuna dawa imeonekana kuwa na uwezo wa kutibu Corona.Ni hatua nzuri kwa nchi za Afrika katika kupambana na ugonjwa huu,"amesema Dk.Migiro.

Kuhusu uwepo wa Tanzania nchini Uingereza wenye kupatwa na maambukizi ya Corona, Balozi Dk.Migiro amesema kwa taarifa ambazo wanazo idadi ya waliopatwa na maambukizi ni Watanzania kati ya 15 na 20.

"Ukweli wapo Watanzania ambao walipatwa na maambukizi ya Corona hapa Uingereza lakini wengi wanaendelea vizuri tu na afya zao zimeendelea kuwa imara,"amesema Dk.Migiro na kuongeza kuwa kwa sasa Uingereza ndio inayoongoza kwa Bara la Ulaya kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages