Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Tom Apson (kushoto), akiwa Hospitali ya Usangi kumjulia hali majeruhi aliyeshambuliwa na mamba katika Ziwa Jipe wakati akivua samaki. Mvuvi huyo amekatwa na mamba nusu ya mkono wake wa kushoto.
Baada ya hapo, DC Apson aliamua kwenda nyumbani kwa majeruhi kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Pia alijumuika na viongozi wa kijiji na kata ya Kigonigoni.
Baada ya hapo, DC Apson aliamua kwenda nyumbani kwa majeruhi kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Pia alijumuika na viongozi wa kijiji na kata ya Kigonigoni.
"Hata hivyo kama Kiongozi Mkuu wa Serikali wilayani Mwanga nimeamua tutasimamia matibabu yake na pia kumsaidia kuanzisha biashara au mradi mwingine atakaoona unafaa baada ya kupona kwake maana amepata ulemavu ambao hautaruhusu aweze kulima au kuvua samaki tena. Mungu amjaalie apone haraka."
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇