Kulingana na taarifa ya Wizara ya afya kuhusu Ugonjwa wa virusi vya corona nchini Tanzania wanaume hao wote wawili waliokufa ni raia wa Tanzania.
Wagonjwa hao ni miongoni mwa wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya covid-19.
Waliothibitishwa kupoteza maisha ni Mwanaume mwenye miaka 51, mtanzania mkazi wa Dar es Salaam na mwanaume wa miaka 57
Halikadhalika wizara ya afya imethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano wa virusi vya corona.
Wagonjwa hao ni wote ni watanzania wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Wagonjwa hao ni wanaume wanne wa miaka 68,54,57 na 41 na mwingine ni mwanamke mwenye miaka 35.
Katika hatua nyingine Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuwepo kwa wagonjwa wengine wawili na kufanya idadi ya walioambukizwa nchini Tanzania kufikia 32, miongoni mwao watano wamepona kabisa.
Waliokutwa na maambukizi baada ya kupokea majibu ya watu waliokuwa wakishukiwa kuwa na maambukizi ni mtanzania mwenye miaka 33 aliyeripotiwa tarehe 7 mwezi Aprili.
Mgonjwa huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kali, mafua na kifua na hivi sasa yuko katika kituo kwa ajili ya uangalizi
Mgonjwa wa pili ni Mtanzania mwenye miaka 24, naye aliripotiwa kuwa na mafua na kikohozi naye alichukuliwa sampuli ambayo imeonesha kuwa ameambukizwa na tayari anaendelea na matibabu.
Wagonjwa hawa wote hawana historia ya kusafiri nje ya nchi kwa siku za hivi karibuni.
Wizara ya afya Zanzibar inaendelea kuwafuatilia watu wa karibu wa wagonjwa hao na wale waliokutana nao ili kudhibiti maambukizi zaidi.
Idadi ya watu walioambukizwa visiwani humo hivi sasa imefikia tisa baada ya ongezeko la wagonjwa hao wawili.
Hatua zilizochukuliwa na Tanzania kudhibiti maambukizi zaidi ya corona:
kufungwa kwa shule zote kuanzia za awali mpaka kidato cha sita kwa siku 30 zikiwa ni jitihada za kudhibiti maambukizi.
Serikali imekua ikiwahamasisha watu kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono ili kuepuka kuambukizwa au kusambaza virusi vya corona.
Wizara ilifanya marekebisho ya ratiba kwa wale wanaotarajiwa kufanya mitihani tarehe 4 Mei, itasogezwa mbele kadiri ya matokeo yatakavyojitokeza ili nao wapate kusoma kwa kipindi kilekile kilichokubalika na ratiba hiyo.
Serikali pia ilisitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile ligi kuu ya Tanzania, Ligi daraja la pili, ligi daraja la kwanza lakini pia michezo ya shule za msingi (UMITASHUMTA), michezo ya shule za sekondari(UMISETA) pamoja na michezo ya mashirika ya umma.
Kuzuwiwa kwa mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇