Mwenyekiti wa NEC, Jajia mstaafu Semistocles Kaijage
Na Richard Mwaikenda
UWEKAJI wazi wa Daftari la Awali na Uboreshaji wa Daftari Wapiga Kura Awamu ya Pili, unaanza rasmi kesho Ijumaa 17 Aprili, 2020. na kukamilika Mei 4, 2020 kwa Nchi nzima.
Na Richard Mwaikenda
UWEKAJI wazi wa Daftari la Awali na Uboreshaji wa Daftari Wapiga Kura Awamu ya Pili, unaanza rasmi kesho Ijumaa 17 Aprili, 2020. na kukamilika Mei 4, 2020 kwa Nchi nzima.
Hayo yametangazwa hivi
karibuni na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu,
Semistocles Kaijage (pichani) wakati wa mkutano na
viongozi wa vyama vya siiasa na wadau wengine kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
Jaji Kaijage, amesema
kuwa,mazoezi hayo yatafanyika kwa siku tatu (3) tu kwenye kila Mkoa na katika route
mbili badala ya route tatu zilizopangwa hapo awali na
yatazingatia, wakati wote, tahadhari zinazoshauriwa na Serikali na Wataalam wa
afya kuhusu mapambano dhidi ya Corona.
Alitaja mikoa mikoa 12 yenye vituo 2005
itakayoanza katika Route ya kwanza inayoanza
kesho Aprili 17 hadi 19
Aprili, 2020, kuwa ni:- Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Mara, Simiyu
na Mwanza. Mikoa mingine ni; Shinyanga, Geita, Kagera, Kigoma
na Tabora.
Route ya pili itakayoanza Mei 02,
hadi 04 Mei 2020, itahusisha Tanzania
Zanzibar na mikoa 14 ya
Tanzania Bara ambapo vituo vya kuandikisha wapiga kura vipatavyo 2001
vitahusika. Mikoa ya Tanzania Bara itakayofikiwa ni Katavi, Rukwa,
Singida, Dodoma, Iringa, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro,
Mbeya, Pwani na Dar es Salaam.
Alitaja vituo vya kuandikisha Wapiga Kura
vitakavyotumika katika Awamu hiyo kuwa ni 4,006, badala ya 8,031 tvilivyotajwa hapo awali. Kati ya hivyo, vituo 3,956
vitakuwa Tanzania Bara na vituo 50
vitakuwa Tanzania Zanzibar.
Aidha Jaji Kaijage amesema kuwa, uboreshaji huo
utafanyika katika kila Kata ambapo kutakuwa na
Mwandishi Msaidizi na BVR Kit Operator watakaowa na orodha ya
vituo vyote katika Kata husika.
Watendaji hao watakuwa na uwezo wa
kuboresha taarifa za Mpiga Kura yeyote
atakayefika kituoni.
Pia, Mpiga Kura
atakayefika kituoni ataandikishwa kulingana na kituo atakachopigia kura siku ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ndani ya Kata husika.
Mpiga Kura ambaye
atakuwa amehakiki taarifa zake na kuhitaji kufanyiwa marekebisho ama Mpiga Kura
anayehitaji kumwekea pingamizi Mpiga Kura mwingine, atatakiwa kwenda kwenye
kituo cha Kata husika kilichopangwa.
Zoezi hili la uwekaji wazi daftari
litawahusu Wapiga Kura wote, wakiwemo wale walioandikishwa mwaka 2015 na wale
walioandikishwa katika awamu ya kwanza ya Uboreshaji.
Aidha, utaratibu wa kuweka pingamizi kwa
aliyeandikishwa utafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 24 (1) cha Sheria ya Taifa
ya Uchaguzi na kifungu cha 30(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa.
Mtu
yeyote ambaye jina lake lipo kwenye Daftari la Awali la Mpiga Kura anaweza
kuweka pingamizi dhidi ya kuendelea kuwepo kwa jina lake mwenyewe au jina la
mtu mwingine yeyote iwapo mtu huyo atakuwa amepoteza sifa za kuwemo kwenye
Daftari au amefariki.
Vilevile, pingamizi
la Uandikishwaji linaweza pia kuwekwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Afisa
Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi.
Mpiga Kura anayetaka
kuweka pingamizi atatakiwa kufika kituoni na kujaza fomu maalum ambayo
inafahamika kama Fomu Na. 3B ambayo, pamoja na mambo mengine, itamtaka atoe
sababu za kuweka pingamizi hilo.
Mweka Pingamizi
anatakiwa kuwasilisha pingamizi ndani ya siku saba (7) kuanzia siku ya mwisho
ya Uwekaji Wazi wa Daftari la Awali katika eneo husika. Pingamizi hilo
litafanyiwa kazi na Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi ndani
ya siku saba (7) na kisha kutolewa uamuzi.
Uamuzi huo unaweza
kukatiwa Rufaa katika Mahakama ya Wilaya na Mahakama hiyo inatakiwa kutoa
uamuzi ndani ya siku 14 tangu tarehe ya Rufaa kupokelewa Mahakamani. Uamuzi wa
mahakama hiyo ni wa mwisho.
Kimsingi, uwekaji
wazi wa Daftari kama ilivyo kwa Uboreshaji wa Daftari utazingatia Sheria za
Uchaguzi na Kanuni zilizotungwa chini ya Sheria hizo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇