Kamati
ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe imeanza utekelezaji wa agizo la
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli la
kuwataka wasafiri waliotoka katika nchi zenye maambukizi ya Virusi vya
Corona kukaa karantini kwa muda wa siku 14 kwa gharama zao.
Mapema leo wajumbe wa Kamati hiyo wametembelea eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia uliopo eneo la Tunduma Mkoani Songwe ili kutathmini utayari wa kuanza zoezi la kuwaweka eneo tengefu yaani karantini wasafiri wote watakaotumia mpaka huo unao julikana kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi nchini kutoka nchi mbalimbali.
Wajumbe hao wamekubaliana kuanza mara moja zoezi la kuwatenga wasafiri wote watakaoingia nchini kupitia Mpaka wa Tunduma kwa gharama zao na kwa muda wa siku 14, ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza leo Machi 23, 2020 usiku huku maandalizi ya maeneo na mahitaji mengine kwaajili ya kuwatenga yakiendelea kufanyika.
Pia wameweka mkakati wa kufanya kaguzi mbalimbali katika nyumba za kulala wageni ili kubaini endapo kuna wageni ambao wataingia nchini kwa kutumia njia zisizo halali na kukwepa kukaa karantini huku ulinzi ukiimarishwa Zaidi katika eneo lote la Mpaka.
Aidha wamewasihi wananchi wote kuendelea kuchukua hatua za tahadhari ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kunawa kwa maji na sabuni, kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima kwani kinga ni bora Zaidi kuliko Tiba.

Eneo la Tunduma ambapo ni Mpaka wa Tanzania na Zambia ambapo wasafiri
wanao toka Nchi zenye Ugonjwa wa Virusi vya Corona kupitia mpaka huo
watawekwa Karantini kwa gharama zao kwa muda wa siku 14.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando akinawa mikono kwa maji yenye
dawa katika Mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma wakati Kamati ya
Ulinzi na Usalama ilipokagua maandalizi ya kuwaweka karantini wasafiri
wanao toka Nchi zenye Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe wakinawa mikono kwa maji
yenye dawa katika Mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma wakati
wakikagua maandalizi ya kuwaweka karantini wasafiri wanao toka Nchi
zenye Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇