LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 24, 2020

HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI WA RUFAA (MST) SEMISTOCLES KAIJAGE KWENYE MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA MWL. NYERERE TAREHE 23 MACHI, 2020

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu mafanikio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Nec, Dk.  Wilson Charles Mahera.



•           Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume,
•           Waheshimiwa Wajumbe wa Tume,
•           Mkurugenzi wa Uchaguzi,
•           Msajili wa Vyama vya Siasa,
•           Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,
•           Viongozi wa Vyama vya Siasa,
•           Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu,
•           Inspekta Jenerali wa Polisi,
•           Kamishna Mkuu wa Uhamiaji
•           Watendaji wa Tume,
•           Waandishi wa Habari,
•           Mabibi na Mabwana

Bwana Asifiwe!!!, Tumsifu Yesu Kristu!!!,  Assalam Aleykum!!!.

Kwanza, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi,naomba kutumia fursa hii, kuwakaribisha katika mkutano huu muhimu ambao madhumuni yake ni kupeana taarifa na kujadiliana kwa pamoja kuhusu kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza. Pia, ni kuwafahamisha kuhusu maandalizi ya zoezi la uwekaji wazi wa Daftari la Awali, pamoja na kuwapa taarifa juu Maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili.

Kama mnavyofahamu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, uandikishaji wa Wapiga Kura na Uwekaji wazi wa Daftari la Awali ni masuala muhimu.

Pili, ningependa nitumie fursa hii, kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa namna ambavyo  mmetoa ushirikiano kwa Tume wakati  wote wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari Awamu ya Kwanza. Niwaombe muendelee kutoa ushirikiano huo katika michakato inayoendelea. Tume inaamini kuwa mafanikio ya mazoezi inayoyaratibu na kuyasimamia yanatokana na ushiriki wa Wadau wa....Inaendelea/Bofya Hapa

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages