Taarifa iliyotolewa na maafisa wa Uingereza imebainisha kuwa, madaktari hao Waislamu waliopoteza maisha katika safu ya mwanzo ya vifo vya madaktari, ni wahajiri. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mmoja wa madaktari hao watatu wa Kiislamu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa Covid-19 kabla ya kuenea virusi hivyo alikuwa akifanya kazi nchini Saudia na Sudan.
Imeendelea kufafanua kuwa, baada ya kuenea virusi vya Corona nchini Uingereza aliamua kurejea nchini humo ili asaidie kutoa huduma za kitaifa katika kukabiliana na maradhi hayo. Hii ni katika hali ambayo wahudumu wa afya katika hospitali za Uingereza hawana mavazi, maski wala vifaa vingine vya tiba vya kutosha kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya Corona, na ni kwa ajili hiyo ndio maana wahudumu wengi wako hatarini kukumbwa na maradhi hayo. Hii ni katika hali ambayo wakuu wa hospitali za nchi hiyo wametahadharisha kwamba, siku chache zijazo vituo vya matibabu nchini humo vitakumbwa na Tsunami ya maambukizi zaidi ya virusi vya Corona.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇