LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 31, 2020

DKT. BASHIRU ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU MKUU CUF

   Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa aliyefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Marehemu Khalifa ambaye enzi ya uhai wake aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Gando, umeswaliwa katika Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu.


Viongozi mbalimbali walihudhuria mazishi hayo akiwamo Dkt. Bashiru ambaye alitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages