LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 17, 2020

ZAIDI YA BILIONI 25 KUTUMIKA MATENGENEZO YABARABARA

Naibu   Waziri   wa   Ujenzi,   Elias   Kwandikwa,   akiruka   katika mtambo wa kuchonga barabara   wakati alipokuwa   akikagua barabara ya Kahama - Solwa -  Mwananga   (km   148)inayokarabatiwa   kwa   kiwango   cha   changarawe,   wilayaniKahama. 

kazi   zikiendelea  za  kukarabati   barabara   ya   Kahama   -   Solwa   -Mwananga   (km   148) kwa  kiwango   cha   changarawe,   wilayaniKahama.
  Muonekano wa sehemu ya barabara   ya   Kahama   -   Solwa   -Mwananga (km 148)  kwa kiwango cha changarawe, Wilaya yaKahama, Mkoa   wa   Shinyanga.   Barabara  hiyo inaunganishawakazi wa Wilaya ya Kahama na mkoa wa Mwanza

Imeelezwa kuwa zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni 25 zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizoathiriwa na mvua nyingi zilizonyesha toka kipindi cha mwisho wa mwaka 2019.

Amezungumza hayo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati akiwa mkoani Shinyanga akiendelea na ziara yake ya kukagua athari za mvua katika miundombinu ya barabara.

Naibu Waziri Kwandikwa amekagua barabara inayotoka Kahama kuelekea Mwananga yenye urefu wa kilometa 148 ambapo sehemu ya barabara hiyo imeathiriwa na maji mengi yanayopita kwenye mkondo wa Ziwa Victoria.

"Hii ni barabara fupi inayounganisha wakazi wa Kahama na Mwanza kupitia Solwa ambapo kilometa 2. 3 ndizo zilizoathirika na hivyo kufanya mawasiliano ya wananchi hawa kuwa ni ya kuzunguka na muda kuongezeka", amesema Naibu Waziri huyo. 

Ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo tayari usanifu wa kina ushafanyika na hivyo Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami.
"Mvua hizi pia zinatupa sisi fursa ya kutazama eneo hili upya kwa kuhakikisha usanifu wetu unaenda sambamba na hali iliyojitokeza na hii itangaliwa maeneo yote nchini", amefafanua Naibu Waziri Kwandikwa.

Ametoa wito kwa wasafirishaji wanaotumia barabara hiyo kutowasumbua wananchi kwa kutumia barabara hiyo na badala yake watumie barabara ya lami ile itokayo Kahama - Isaka - Tinde mpaka  Mwanza kwa kuwa inapitika vizuri kabisa.
Aidha, ameeleza mkakati wa Serikali katika kipindi hiki cha mvua kuwa inaendelea kufuatilia maeneo yote ambayo ni korofi na kuona namna nzuri ambayo inaweza kufanya ili kuwanusuru wananchi kuondokana na adha hizo na waweze kuendelea kupata huduma mbalimbali kwa kutumia barabara.

wananchi kuondokana na adha hizo na waweze kuendelea kupatahuduma mbalimbali kwa kutumia barabara.Kwandikwa amewahakikishia wananchi wa  maeneo yote nchiniambao   wameathiriwa   na   uharibifu   wa   mvua   hizi   katikamiundombinu ya barabara kurejeshewa kwa mawasiliano katikamaeneo   hayo   huku   mwarobaini   wa   maeneo   hayo   koro2ukiandaliwa."Niwahakikishie   wananchi   kuwa   Serikali   yao   iko   makini,inasimamia rasilimali zote kwa makini na inakusanya fedha kwaajili ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi",amesema NaibuWaziri Kwandikwa.


 Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Matengenezo kutoka Wakalawa   Barabara   (TANROADS),mkoa   wa   Shinyanga   MhandisiFrednand  Mdoe,  ameeleza  kuwa  wanapata  changamoto  kubwaya kurudisha mawasiliano katika barabara hiyo kutokana na majikuzidi   kuongezeka   na   tayari   washakusanya   mawe   kwa   ajili   yakurudisha barabara hiyo ili iweze kupitika."Huu ni mkondo wa Ziwa hivyo maji yamekuwa mengi na kuvukabarabara  na  kasi  ya  kupungua   kwa  maji  haya imekuwa  ndogolakini   tumejipanga   mipango   ya   sasa   na   mipango   ya   kudumuambayo ni ujenzi wa madaraja katika barabara hii katika mwakawa fedha unaokuja", amesema Mhandisi Mdoe.Naibu   Waziri   Kwandikwa   yupo   katika   ziara   ya   kikazi   mkoaniShinyanga ya kukagua athari za mvua zinazoendelea kunyeshahapa   nchini   na   kusababisha   uharibifu   wa   miundombinu   yabarabara.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages