LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 17, 2020

PROF. ANNA TIBAIJUKA APONGEZA KUPUNGUA KWA MIMBA WANAFUNZI KAGERA

Sehemu ya matembezi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilayani Muleba Athuman Kahara akizungumza na wananchi
Mbunge wa Muleba kusini mkoani Kagera Prof Anna Tibaijuka akizungumza na wananchi wake

Na Lydia Lugakila Kagera:-

Mbunge wa Muleba kusini mkoani Kagera Prof Anna Tibaijuka kwa kushirikiana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo wamepongeza juhudi za Mwalimu Catherine ambaye ni mkuu wa shule ya Sekondari Rukindo  iliyopo wilayani  humo kwa kusimamia vema suala la mimba kwa wanafunzi huku kiwango hicho kikitajwa kushuka kutoka mimba 26 mwaka 2019 hadi mimba 4 kwa mwaka huu 2020.

Prof Anna Tibaijuka ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa ametembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo barabara na hospitali ya Buganguzi iliyopo wilayani humo sambamba na kuongea na wananchi.

Prof Tibaijuka akiwa ameambatana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM  Athumani Kahara wametembelea miradi hiyo ya maendeleo  ambapo Mbunge huyo ameongea na wananchi na kumpongeza Mwalimu Catherine ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari ya Rukindo kwa juhudi za kusimamia suala la mimba shuleni hapo ambalo lilisababisha kuwepo kwa mimba 26 mwaka 2019 na mwaka huu wa 2020 kupungua hadi kufikia mimba 4.

Mbunge huyo amesema hali hiyo yenye mafanikio imekuja kutokana na Mwalimu huyo kusimamia vema suala hilo ambalo alihakikisha wanafunzi hao wanapimwa kila baada ya miezi mitatu.

Prof Tibaijuka amesema kutokana na jitihada hizo za mwalimu hataki kuona au kusikia wazazi wa wanafunzi hao wanamsumbua bali wanapaswa kutoa ushirikiano mkubwa.

Prof huyo pia ametoa shukrani kwa Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani humo Athuman Kahara kwa kusimamia shughuli za maendeleo.

Aidha amempongeza Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo ametekeleza na kufanikisha maendeleo kwa wananchi wake.

Katika hatua nyingine amewahimiza vijana kuomba mikopo na kufanya kazi kuliko kutegemea shughuli moja ya kuendesha piki piki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilayani humo Athuman Kahara amekemea wenyeviti wa vijiji wanaojihusisha na uuzaji wa ardhi ya kijiji kuacha Mara moja suala hilo vinginevyo wataondolewa katika nafasi zao.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages