Na Lydia Lugakila:- Kagera.
Waziri mkuu wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili mkoani kwa ziara ya siku mbili kwa ajili ya shughuli za kiserikali pamoja na za chama cha mapinduzi CCM.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti katika kikao na waandishi wa habari katika ofisi za mkoa huo.
Akitoa taarifa za ujio wa Waziri mkuu , mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema waziri Majaliwa atawasili mkoani Kagera mnamo Februari 20 mwaka huu majira ya Saa 3 :30 asubuhi kwa ajili ya shughuli maalum za chama cha mapinduzi CCM pamoja na shughuli nyinginezo za serikali ikiwemo kupewa taarifa ya mkoa huo ambapo shughuli zote hizo zitafanyika kwa siku mbili Februari 20 -21 mwaka huu
Brigedia Marco Gaguti amesema Waziri huyo atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Bukoba.
Mkuu huyo ameeleza kuwa waziri mkuu ambaye pia ni mlezi wa chama cha mapinduzi CCM atapata nafasi ya kuongea na viongozi wa chama hicho katika vikao vya ndani vya chama hicho.
Hata hivyo ameongeza kuwa endapo itatokea mabadiliko mengine ikiwemo kukutana na wananchi taarifa zitatolewa na uongozi wa mkoa.
Your Ad Spot
Feb 19, 2020
WAZIRI MKUU ATARAJIWA KUWASILI MKOANI KAGERA KWA ZIARA YA KIKAZI
Tags
featured#
habari picha#
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
habari picha
Tags
featured,
habari picha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇