Mratibu wa mafunzo Bi. Laura Marandu (kulia) kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya akizungumza jambo na Walimu wa Vyuo vya Afya katika Ukumbi wa CEEMI, NIMR Mkoani Dar es Salaam.
Walimu wa Vyuo vya Afya wakifurahia jambo wakipiga makofi wakati Mkutano ulipokuwa ukiendelea katika Ukumbi wa CEEMI, NIMR Mkoani Dar es Salaam.
Walimu wa Vyuo vya Afya wakifurahia jambo wakipiga makofi wakati Mkutano ulipokuwa ukiendelea katika Ukumbi wa CEEMI, NIMR Mkoani Dar es Salaam. |
Mratibu wa mafunzo Bi. Laura Marandu (kulia) kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya akizungumza jambo na Mshauri Mwandamizi wa Udhibiti na kuzuia maambukizi mradi wa MTaPS Dkt. Doris Lutkam
Walimu wa Vyuo vya Afya wakisikiliza kwa makini
Picha ya pamoja ya Walimu wa Vyuo vya Afya, Tanzania
|
Mafunzo ya Mwongozo wa Kukinga na Kudhibiti Maambukizi katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya yatolewa kwa Walimu wa Vyuo vya Afya, Tanzania tarehe17-22 Februari 2020 katika Ukumbi wa CEEMI, NIMR Mkoani Dar es Salaam.
Mafunzo haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) kupitia Kitengo cha Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya (HQAU) kwa kushirikiana na Idara ya Mafunzo (DHRD) kwa udhamini wa Shirika lisilo la Kiserikali la Medicines Technologies and Pharmaceutical Services (USAID-MTaPS).
Jumla ya washiriki 31 wamepata mafunzo kutoka Vyuo vya Wauguzi na Wakunga, Wataalamu wa Maabara, Mazingira na Matabibu (CO). Aidha, waalimu hawa walipata fursa ya kukumbushwa mbinu mbalimbali za kufundisha na baadae walionesha umahiri wao kwa kufundisha kwa kufuata yale waliyofundishwa mbele ya wenzao na wakufunzi.
Nae Mratibu wa mafunzo hayo Bi. Laura Marandu kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya aliwasisitizia washiriki kuhakikisha kuwa wanawafundisha wanavyuo pamoja na watumishi kutoka katika hospitali zao namna ya kujikinga maambukizi katika vituo vya kutolea huduma za afya, kushiriki katika zoezi la usimamizi wa ndani (internal auditing) ili kuibua changamoto katika masuala ya kukinga na kudhibiti maambukizi ili kujiwekea mikakati ya namna bora ya kutanzua changamoto hizo kuanzia chuoni hadi katika uongozi wa hospitali zao.
Alisisitiza kuwa, waalimu ndio wanaowaandaa watumishi wajao hivyo wasione haya kuwarekebisha na kushauri hata watumishi wanapokuwa wanatoa huduma kinyume na miongozo na viwango vya utoaji huduma vilivyowekwa.
Alisema Bi. Marandu kuwa, yapo magonjwa yaliyokuwepo na mengine mapya yanayoibuka ambayo ni hatarishi lakini kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile kunawa mikono, kutumia vifaa maalumu vya kujikinga na maambukizi, matumizi sahihi ya viua vijasumu (antibiotics) kutaepusha usugu wa vijidudu dhidi ya viua vijasumu, kupatwa au kusambaa kwa maambukizi ya maradhi endapo magonjwa hayo yataibuka.
Aliendelea kusisitiza kuwa masuala ya kujikinga na kudhibiti maambukizi ni jukumu la kila mtumishi anaefanya kazi katika vituo vya kutolea huduma za afya kama vile Watumishi wa Vyumba vya kutunzia Maiti, Dobi, Wauguzi, Madaktari, Wafamasia,wataalam wa maabara, wanaotoa huduma ya chakula na wanaofanya usafi wa mazingira hata kama wameajiriwa na kampuni lazima wapewe mafunzo ya kujikinga dhidi ya maambukizi vituoni.
Bi. Marandu aliwaelekeza walimu kuwa miongozo na nyaraka mbalimbali za WAMJW zinapatikana katika tovuti www.moh.go.tz au www.tzdpg.or.tz pia, waalimu waaligawiwa Mwongozo wa Kukinga na Kudhibiti Maambukizi (2018) na Mwongozo wa Mshiriki (participants manual) ambavyo wanapaswa kuvitumia katika maktaba za vyuo na hospitali zao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇