Vikosi vya Marekani na Afghanistan jana vimeshambuliwa katika eneo la mashariki mwa jimbo la Nangarhar nchini Afghanistan. Taarifa ya jeshi la Marekani kutoka Kabul inasema vikosi hivyo ambavyo vinashiriki katika operesheni katika jimbo hilo vilikabiliwa na shambulizi la moja kwa moja. Msemaji wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan Kanali Sonny Leggett pasipo kutoa taarifa za kina alisema wanaitathimini hali ilivyo na watatoa taarifa zitakavyopatikana. Nangarhar ni moja kati ya majimbo tete mashariki mwa Afghanistan, ambako Kundi la Taliban na Dola la Kiislamu yana nguvu. Mwaka uliopita wanajeshi 20 wa Marekani walikufa katika operesheni ya kijeshi inyaofanana na tukio hilo la sasa.
Your Ad Spot
Feb 9, 2020
WANAJESHI WA MAREKANI NA AFGHANISTAN WASHAMBULIWA
Tags
featured#
Kimataifa#
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇