LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 3, 2020

SAMATTA AWEKA REKODI MBILI ENGLAND ASTON VILLA IKICHAPWA 2-1 NA BOURNEMOUTH VITALITY


Na Mwandshi Wetu, BOURNEMOUTH 

MSHAMBULIAJI Mbwana Ally Samatta leo ameweka rekodi mbili kwa mpigo, kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza na kufunga kwenye Ligi Kuu ya England, timu yake mpya, Aston Villa ikichapwa 2-1 na wenyeji, AFC Bournemouth Uwanja wa Vitality.
  Samatta aliyekuwa anacheza mechi yake ya pili tu Villa baada ya uhamisho wa Pauni Milioni 8.5 kutoka KRC Genk ya Ubelgiji, alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 70. 
  Na hiyo ilifuatia wenyeji, AFC Bournemouth iliyomaliza pungufu baada ya Jefferson Lerma kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 51, kutangulia kwa mabao ya kiungo wa kimataifa wa Denmark, Philip Billing dakika ya 37 na beki Mholanzi, Nathan Ake dakika ya 44.

Mbwana Samatta mekuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza na kufunga kwenye Ligi Kuu ya England 

The Cherries wanapanda hadi nafasi ya 16 baada ya ushindi huo wakifikisha pointi26 katika mchezo wa 25, wakati Villa inaangukia nafasi ya 17 ikibaki na pointi zake 25 za mechi 25 pia.
  Samatta aliichezea Villa kwa mara ya kwanza Jumanne ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi Leicester City kwenye mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi na kufankiwa kuingia fainali na sasa itamenyana na Manchester City Machi 1 Uwanja wa Wembley.  
  Kikosi cha AFC Bournemouth kilikuwa; Ramsdale, Smith, Francis, Ake, Rico, Gosling, Lerma, Billing, H Wilson, C Wilson na Fraser.
  Aston Villa: Reina, Hause, Mings, Konsa/Engels dk46, Guilbert, Luis, Nakamba/Trezeguet, Targett, Grealish, Samatta na Al Ghazi/Davis. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages